Zinazobamba

TCRA YAWAFUNDA WAANDAA VIPINDI VYA RADIO NA TV, YAWATAKA KUWEKA MASLAHI YA TAIFA MBELE,

Mkurugenzi wa idara ya utangazaji  mamlaka ya mawasiliano , akifafanua  kanuni za utangazaji za mwaka 2005 kwa wahariri na watayarishaji mapema hii leo, Mkurugenzi huyo amewataka wahariri hao kujenga tabia ya kuandaa maudhui yenye tija kwa taifa kwani kwa kufanya hivyo itasaidia vizazi vyetu kuwa na tabia yenye maadili mema

 Mamlaka ya mawasiliano hapa nchini,imewataka waanda vipindi katika vituo mbalimbali vya radio na televisin hapa nchini kuacha kuiga mkumbo kwa kuandaa maudhui ambayo hayana tija kwa taifa , na badala yake wajikite katika kuaandaa maudhui itakayochochea kuongezeka kwa vitendo vyema ndani ya jamii,

Akizungumza na waandaa maudhui hao hapa nchini, mkurugenzi mtendaji wa utangazaji katika malaka hiyo, Ndg,Habib Gunze amesema ili kuwa na jamii inayoheshimu maadili, basi radio na television vinamchango mkubwa sana wa kubadilisha maadili kwa kuandaa maudhui yenye tija kwa Taifa,
Gunze amesema, machafuko mara nyingi yanaasababishwa na maudhui ya radio katika jamii husika, kwani radio inauwezo wa kujenga ama kubomoa jamii inayowazunguka

Mwenyekiti wa kamati ya maudhui ya TCRA, Mhandisi Margaret Tabu Munyagi, akifafanua jambo mbele ya wahariri na watayarishaji wa vipindi vya vyombo vya utangazi vya kanda ya mashariki. Katika warsha hiyo ya siku moja Mwenyekiti huyo amewataka wahariri na watayarishaji hao kuwa makini na maudhui wanayoyaruhusu kwenda hewani, kwani wao ni watu muhimu sana kwa kujenga jamii yenye maadili mema.
Baadhi ya wahariri waliohudhulia warsha hiyo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti kuhusiana na mada aliyokuwa anaiwasilisha kwao, wahariri hao wameonyesha  kuguswa na ushirikiano ulioanzishwa na mamlaka hao kwa kitendo cha kuwafanya wahariri hao kuwa karibu na mamlaka, wakisema huo ni mwanzo mzuri wa kuhakikisha maudhui yatakayokuwa yakienda hewani yanafuata maadili ya taifa hili.

Mmoja wa wahariri maarufu toka mkoani morogoro aliyefahamika kwa jina la jafari mponda, akisikiliza kwa makini hutuba ya mwenyekiti,



Mwanasheria wa mamlaka ya mawasiliano hapa nchini, akifafanua hatua za upatikanaji wa leseni za ueendeshaji wa vituo vya redio na television zake, Mwanasheria huyo amewataka wahariri hao kufuata sherria za utangazaji ili wasiweze kumuonea mtu katika kutangaza maudhui yao, amesema stori itakayotangazwa ni lazima iwe imefuata  taaluma ya uandishi wa habari

Mmoja wa wadau wa mkutano huo akichanga moja ya mada zilizowasilishwa katika mkutano huo, Mama huo amesema tatizo la ajira kwa waandishi wa habari bado kitendawili na kivipi mamlaka imejipanga kuwasaidia waandishi, jibu alilojibiwa ni kwamba mshahara unapangwa na bosi wake, mamlaka inakazi tu ya kushauri

Wadau toka mkoani Morogoro wakipozi kwa picha baada ya kuhitisha zoezi la mkutano.

No comments