Zinazobamba

uhuru wa habari kikaangoni, ITV, STAR TV na radio Free Afrika vyanusurika kufungiwa maisha...

 


KATIKA kile kinachodaiwa kuwa .ukandamizwaji wa haki ya uandishi wa habari hapa nchini unaofanywa na vyombo vya dolla, Mamlaka ya mawasiliano kupitia kamati yake ya maudhui leo hii imeonyesha dhahili shahiri kuwa uhuru wa vyombo vya habari sasa ni historia katika taifa la Tanzanaia baada ya kuvivaa vyombo maarufu hapa nchini na kuvipa onyo kali pamoja na kutoa muongozo wa program zao kabla ya kuzitangaza


Hatua hiyo imekuja baada ya Kituo cha  Indipendent Television (ITV) na kituo cha matangazzo cha Sahara media communication kutangaza Matangazo yanayodaiwa na malaka ya mawasiliano Tanzania kuwa yamekiuka maadili ya Utangazaji na kupewa Onyo kali dhidi ya vyombo hivyo.
MENEJA UTAFITI NA MIPANGO W KAMPUNI YA SAHARA MEDIA BW. NATHAN LWEHABURA AKIFAFANUA JAMBO BAADA YA KUPOKEA HUKUMU YAO,



Akisoma hukumu dhidi ya vyombo vya habari vya ITV, STAR TV na Radio Free Africa, mwenyekiti wa kamati ya maudhui katika mamlaka hiyo, Bi.Magrete Munyagi Amesema kuwa vituo hivyo vya habari vimekiuka maadili ya utangazaji na kwamba kamati hiyo imetoa huku kwa kuwapa onyo kali ikienda sambamba na kuwasilisha katika mamlaka hiyo miongozo yao ya namna wanavyochuja maudhui kabla ya kuyatangaza

Munyagi amesema kuwa kwa sasa kwa kuwa wamiliki wa vyombo hivyo vimekiri uwepo wa makosa yao kwa kurusha maudhui ambayo hayana tija kwa taifa, hivyo kamati imeamua kutoa Onyo kali kwa vyombo hivyo, na kwamba wakirudia tena basi adhabu kali itachukua mkondo wake
Katika hatua nyingine, meneja utafiti na mipango wa kampuni ya sahara media ,Bw. Nathan Lwehabura amesema kuwa onyo walilopewa haliishii tu kwa ITV, STAR TV na Radio free afrika na badala yake, tasnia nzima lazima tuwe makini katika suala zima la maudhui,
MWENYEKITI WA KAMATI YA MAUDHUI, AKISAINI HUKUMU ZILIZOTOLEWA KWA VYOMBO VYA HABARI VYA ITV NA STAR TV, KATIKA HUKUMU HIYO, VYOMBO HIVYO VIMEPEWA ONYO KALI

Yaliyotupata sisi leo sio kwamba ni peke yetu, hiyo ni kwa vyombo vyote hapa nchini pamoja na waandishi wa habari wenyewe kwani ukiona mwenzio kanyolewa wewe tia maji,
Wadadisi wa habari hapa nchini wameichukulia hatua hiyo kama changamoto kwa vyombo vya habari na waandishi wenyewe, kwani kwa sasa inaonekana wazi kuwa tasinia ya habari uhuru wake unaanza kubanwa kila kona,
 
Joyce Mhavile akipokea huku yao iliyotolewa na kamati ya maudhui kwa kitu cha ITV, JOYCE MHAVILE ni mkurugenzi wa kituo cha ITV
Angalia kule bungeni, waandishi wa habari hawana thamani kabisa, wamekuwa kama watu ambao hawana mchango wowote katika suala la katiba, baada ya kunyimwa haki ya kuingia katika kamati za bunge maalum la katiba, aliongeza mmoja wa wadau waliozungumza na mtandao huu hivi karibuni.


wajumbe wakiwajibika, katika hukumu hyo
 
WAjumbe wa kamati ya maudhui wakifuatilia kwa makini hukumu inayosomwa na mwenyekiti wa kamati hiyo mapema hii leo
MKURUGENZI WA MAMBO YA UTANGAZAJI  KATIKA MAMLAKA YA MAWASILIANO, AKIFUATILIA KWA MAKINI HUKU INAYOTOLEWA DHIDI YA VYOMBO VYA HABARI VYA ITV STAR TV NA REDIO FREE AFRICA

No comments