UGANDA YAPUNGUZIWA MISAADA KUTOKANA NA SHERIA DHIDI YA MASHOGA
Wakati Serikali za Marekani, Sweden na Japan zikitafakari hatua za
kuchukua dhidi ya Serikali ya Uganda; Denmark na Norway zimesema
zinapunguza mamilioni ya dola za msaada kwa Serikali ya Uganda kufuatia
Serikali ya nchi hiyo kupitisha sheria mpya dhidi ya vitendo vya
kishoga.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amehusisha sheria mpya ya Uganda dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na ubaguzi wa rangi katika enzi za Nazi na Afrika Kusini.
Amesema sheria hizo za kupinga wapenzi wa jinsia zimeibua hisia mbalimbali Marekani na kusababisha changamoto kwa sababu haki za mashoga ni haki za kibinadamu.
Thamani ya shilingi ya Uganda ilishuka kwa zaidi ya asilimia 2 Jumatano, siku mbili baada ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni kutia saini sheria hiyo yenye adhabu kali kwa wapenzi wa jinsia moja Jumatatu
Sheria hiyo mpya imepiga marufuku uhamasishaji wa mapenzi ya watu wa jinsia moja na wale wote wanaojihusisha na maswala ya ushoga wanaweza kukabiliwa na adhabu ya kifungo cha maisha jela.

No comments
Post a Comment