Zinazobamba

LHRC WAJITOSA MAPIGANO YA WAKULIMA WAFUGAJI KITETO ,, WAITAKA SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU WATENDAJI MIZIGO,

 
 Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini tanzania leo kimeitaka
    serikali kuwachukulia hatua kali za kinidhamu  mkuu wa mkoa wa manyara,mkuu wa wilaya ya kiteto pamoja na mkurugunzi wa wilaya ya kiteto baada ya kugundua kuwa wao ndio chanzo kikubwa cha mgogoro wa wakulima na wafugaji uliotokea mapema mwaka huu na kugharimu maisha ya watu.

 Akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam wakati akitoa tamko la kituo hiko kuhusu mgogoro huo wakili EMELDA URIO amesema kuwa kituo hiko kimegundua kuwa viongozi hao ndio chanzo kikubwa cha  mgogoro huo baada ya kuruhusu ukusanyaji wa fedha usio wa halali  kutoka kwa wafugaji ili kulipia gharama za dalali wa kuwaondoa wakulima katika eneo lenye mgogoro jambo ambalo amesema kuwa lilizua taharuki kubwa na baadae mapigano makubwa sana
             Aidha amezitaja sababu nyingine zilizochangia mgogoro huo kuwa ni mfumo mbovu wa matumizi ya ardhi ya kijiji kwani wale ambao wanaonekana ni wavamizi walipata ardhi maeneo hayo kutoka kwa viongozi wa kijiji kwa kutoa kiasi fulani cha fedha.

WAKILI EMELDA URIO AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA WAAANDISHI WA HABARI MAPEMA HII LEO

           Katika hatua nyingine kituo cha sheria na haki za binadamu
    kimelitaka jeshi la polisi kuhakikisha kinafwatilia kwa makini
    mgogoro huo na kuhakikisha kuwa linawachukulia hatua kali za
    kisheria wale wote wanaotajwa kuhusika katika mgogoro huo.


No comments