ccm na walaka wake,
Waraka huo wa kurasa 22 unaoainisha mambo yenye masilahi kwa chama hicho, unawataka wajumbe wake kuutetea bungeni.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.PICHA|MAKTABA
Gazeti hili limefanikiwa kuona waraka huo, ambao pamoja na mambo
mengine, umetoa mapendekezo katika ibara 42 za Rasimu ya Katiba ya Tume
na kupangua hoja nyingi.
Katika miongoni mwa hoja hizo, chama hicho kimesisitiza muundo wa
Muungano wa Serikali mbili lakini kikapendekeza kuwapo Baraza la
Wawakilishi la Tanzania Bara.
Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu waraka huo, Katibu wa Itikadi na Uenezi
wa CCM, Nape Nnauye aliukana akisema pamoja na msimamo wa chama hicho
kuwa ni Serikali mbili, hakijafikia hatua ya kuwa na waraka.
Alisema vikao vya juu vya chama huwa havitoi waraka, bali msimamo na
kwamba vyombo vingine vya chama ndivyo hutoa waraka, lakini hadi sasa
havijafikia hatua hiyo.
Alisema kuwa alipoeleza maazimio ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM
(NEC), alitaja msimamo wa chama hicho kuwa ni Serikali mbili
zilizoboreshwa, lakini hakutaja maboresho hayo hata pale alipoulizwa na
waandishi wa habari kwa sababu hayakuwa yamekamilika.
Hata hivyo, wajumbe watatu wa NEC kwa nyakati tofauti waliomba wasitajwe
gazetini walisema mambo yaliyomo kwenye waraka huo ndiyo
waliyokubaliana lakini hakuwa na uhakika kama ulishasambazwa.
No comments
Post a Comment