MATHAYO AKABIDHI OFISI RASMI, AKILI WIZARA KUWA NA CHANGAMOTO LUKUKI, ALI
Aliyekuwa waziri wa wizara ya mifugo na uvuvi, Mh. David Mathayo David amekabidhi rasmi ofisi yake kwa waziri mteule mpya ili kuendelea na majukumu ya kuiongoza waizara hiyo ambayo imekubwa na migogoro mbalimbali ikiwemo ile ya wakulima na wafugaji ambao kila leo tumeshuhudia wakiuana,
Akikabidhi ofisi hizo mapema hii leo jiji Darsalaam, Mathayo amekili kuwepo kwa changamoto mbalimbali ambazo zinahitaji kuchukuliwa hatua haraka iwezekanavyo ili kuwanusuru watanzania wengi wanaofariki kutokana na migogoro isiyo na tija,
Akitaja changamoto ambayo ni sugu, katika wizara hiyo ni vita iliyopo ya maeneo kati ya wakulima na wafugaji ambayo kwa muda mrefu tatitizo hilo limeshindwa kupatiwa ufumbuzi
Amesema kijiti ambacho anamuachia Titus Kamani, ni kigumu na kwamba ni lazima awe tayari kuona ni namna gani anavyoweza kupambana na changamoto zitakazojitokeza mbele yake
| Aliyekuwa waziri wa Wizara ya mifugo na uvuvi akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari katika makabidhiano ya nyaraka za serikali kwa waziri mpya ambae amempokea kijiti |
| baadhi ya watendaji wakijiinamia chini katika hafla hiyo, matahayo amekabidhi nyara zote muhimu |
| Waziri mteule mpyaMh. Dr. Titus Mlengeya Kamani (kushoto) akipokea nyaraka muhimu za kufanyia kazi toka kwa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo mh. David Mathayo.Davidmapema hii leo |
| baada ya makabidhiano ya fisi ilifika wakati wa kuweka kumbukumbu, hapa waziri Mathayo akipiga picha ya pamoja na waziri mpya pamoja na uongozi mzima wa wizara ya mifugo na uvuvi |
No comments
Post a Comment