LOWASA NA MATUMAINI YA URAIS 2015, asema "Nimeanza safari yenye matumaini makubwa kwa Watanzania kwa kuwa itakuwa na elimu bure, maji safi na salama na huduma za afya zenye uhakika"...

Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametangaza kuanza rasmi kwa safari
aliyoiita ya matumaini ya ndoto zake, ambayo amesema itatimiza ndoto za
Watanzania za kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika.
Akizungumza
katika ibada ya shukrani na kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Usharika ya Monduli Mjini, Lowassa
bila ya kutaja safari hiyo ni ipi, aliwashukuru watu wote kutoka maeneo
mbalimbali nchini, ambao walimsindikiza katika ibada hiyo.
Lowassa
alisema anaamini watu hao waliofika, wana uhakika wa ushindi katika
safari hiyo kwa kumtegemea Mungu.
Licha ya
kutoweka bayana, Lowassa amekuwa akitajwa kuwa ni mmoja wa wanasiasa
wanaowania kumrithi Rais Jakaya Kikwete baada ya kumaliza kipindi chake
cha uongozi mwakani.
Azungumzia
Katiba Mpya.
Akizungumzia
Katiba Mpya, ambayo mchakato wake sasa unaelekea katika Bunge Maalumu,
licha ya kuipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Mwenyekiti
wake, Jaji Joseph Warioba alisema ana wasiwasi juu ya muundo wa Serikali
Tatu.
"Nina
wasiwasi na huu muundo, ni vyema viongozi wa dini, kuliombea taifa
tupate Katiba bora kwani maoni ya watu asilimia 40 ambao hawakutaka
muundo wa Serikali Tatu lazima yatazamwe," alisema Lowassa.
Ibada
katika Kanisa hilo, ambayo iliendana na harambee ya kuchangia hosteli na
zaidi ya Sh89 milioni kupatikana, iliongozwa na Kaimu Askofu wa KKKT,
Usharika wa Kaskazini Kati, Solomon Masango.
Katika
mahubiri yake, Kaimu Askofu Masango alimtakia kila la heri Lowassa
katika safari yake hiyo akisema anamtambua kuwa ni kiongozi bora.
Hafla ya
nyumbani
Akizungumza
katika hafla aliyoandaa baadaye nyumbani kwake, Lowassa alirudia kauli
yake ya kuanza safari.Waliohudhuria halfa hiyo ni pamoja na wabunge
wengi wakiwa wa CCM, wenyeviti wa CCM, wakiongozwa na Mwenyekiti wa
Wenyeviti wa CCM, Mgana Msindai kutoka Mkoa wa Singida, Mwenyekiti wa
Wenyeviti wa UVCCM, Manka Dilu kutoka Mkoa wa Mara na Mwenyekiti wa
Wenyeviti wa Wanawake wa CCM, Diana Chilolo pia kutoka Mkoa wa Singida,
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara, Lucas ole Mukusi ambaye ndiye katibu
wa wenyeviti wote wa CCM.
Wengine
waliohudhuria ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), mikoa
mbalimbali ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM na viongozi wa dini
mbalimbali. Pia alikuwapo aliyekuwa mgombea urais wa Kenya katika
uchaguzi uliopita, Profesa James ole Kiapi.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Lowassa alisema ndoto ya elimu bure, ajira kwa
vijana, kuondoa umaskini zitafanikiwa baada ya kuanza safari yake hiyo
hapo jana.
Alisema
wakati ukifika wa kutangaza rasmi nia hiyo, ataeleza mengi na akawataka
wanaomuunga mkono wasiwe na shaka... "WanaCCM msiwe na shaka, tutavuka
kwa nguvu zetu... wingi wenu huu unanipa faraja kuwa katika safari yetu
na kwa kumtegemea Mungu tutashinda."
Lowassa
aliwataka waungane na kaulimbiu yake, 'Tulifurahi pamoja, tulihuzunika
pamoja na tutashinda pamoja' na baada ya kusema maneno hayo, alipokewa
kwa sauti za CCM... CCM... CCM.
Waalikwa
wazungumza
Akizungumza
katika hafla hiyo, Msindai ambaye aliwaongoza wenzake Mwenyekiti wa CCM
Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja na Onesmo Nangole wa Mkoa wa Arusha
alisema wanamuunga mkono, Lowassa katika safari yake hiyo.
Alisema
anamfahamu Lowassa kwa muda mrefu na kumwelezea kwamba ni kiongozi bora
mwenye uamuzi na kwamba haoni sababu ya kutokumuunga mkono.
Mgeja
alisema anawashangaa watu wachache ambao wameanza tabia ya kulazimisha
watu kuwachagulia marafiki na kuwachafua wengine.
Alisema
hakuna ambaye hafahamu kuwa Lowassa ndiye tumaini la Watanzania akisema
jina lake linatajwa kila kona kwa kuwa ana uwezo na sababu za kuwa
kiongozi wa Taifa.
Mgeja
alionya kuwa kuna kundi la watu linalodhani kuwa CCM ni mali ya viongozi
kitu ambacho alisema si sahihi, bali ni mali ya wanachama ambao alisema
ndiyo wenye uamuzi.
Nangole
alisema Lowassa ni kiongozi msikivu na makini ambaye ni tegemeo la
Watanzania katika kuwaunganisha kuwa kitu kimoja.Wakizungumza katika
hafla hiyo, viongozi hao wa CCM, walisema wanamuunga mkono Lowassa
kutokana na uwezo mkubwa alionao.
Manko kwa
upande wake alisema UVCCM ina imani kubwa na Lowassa kwani ni mmoja wa
makada wa CCM wenye historia ndefu katika chama hicho.
Kwa
upande wake, Mbunge wa Chemba Kondoa (CCM), Juma Nkamia alisema Lowassa
sasa ni sawa na Simba na kusema wanaomchukia walie tu kwani ni kiongozi
bora.
Mjumbe wa
Baraza Kuu la UVCCM, Hussein Bashe aliwataka wananchi wa Monduli
kutunza heshima ya Lowassa na kwamba kazi nyingine watafanya wao.
Alisema
safari ya Lowassa ndiyo, imeanza inawezekana na kwamba alipoanguka mwaka
2008, ilikuwa ni mipango ya Mungu kuwezesha safari hiyo. "Lowassa ana
sifa zote za uongozi... tunachokiomba kwenu ni ushirikiano tu."CHANZO
MWANANCHI
No comments
Post a Comment