Zinazobamba

LOWASA ATIMULIWA CCM,Wenyewe wasema akibaki chama kwisha habari yake

Nikama yametia hivi,Umoja wa vijana ccm, Umemtaka kada wa CCM hapa nchini, na Mbunge wa Monduri Mh. Edward Lowasa kutafakari na kujitathmini kama anafaa kuendelea kukitumikia chama, ama ang'atuke kupisha watu wenye moyo wa kuwatetea wananchi kuchukua nafasi zao
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo, katibu wa UVCCM taifa, amesema hatua hiyo imekuja kufuataia mwenendo wa kiongozi huyo anayeheshimika na watu wengi, kuwa mbovu ndani ya Chama

Katibu huyo amesema LOWASA anatumia vibaraka wake kuhakikisha anakichonganisha Chama, kwa kupeleka na kuongea maneno ambayo hayana ukweli wowote katika vyombo vya habari, maneno ambayo yanalenga kukirarua chama chenye nia njema ya kuwatetea wananchi

Amesema hakuna asiyejua kazi nzuri iliyofanya na viongozi wa Kitaifa wa CCM, huko mikoani, lakini leo hii vibaraka wa Lowasa wanajitokeza mbele na kuanza kuchonganisha chama na serikali iliyo madarakani pamoja na wananchi, hali hiyo haikubaliki hata kidogo aliongeza katibu huyo

Katika hatua nyingie katibu huyo ametoa wito, kwa wananchi wa tanzania, maaskofu, mashehe na vijana kwa ujumla wawasaidie CCM kwenda kuchukua fedha za mchezo ambazo LOwasa anatoa kila leo kwa wdau mbalimbali

"Ndugu zangu watanzania kama mnataka fedha za haraka nendeni kwa lowasa anazo pesa nyingi sana anagawa akidhani zitampeleka ikulu, sasa chukueni pesa zake ili ziwasaidie ila sifa za kuwa Rais Lowasa amepoteza na CCM tupo macho juu ya hilo" alisema

Sisi kama vijana ambao tunafikili kwa kutumia akili na sio Tumbo, hatuwezi kukaa kimya huku tukiona viongozi wetu wa juu wakisemwa vibaya juu ya kazi nzuri waliyofanya katika ziara yao ya mikoani,

Leo hii anakurupuka mtu na kuanza kuropoka katika vyombo vya habari vitu vya kubomoa chama, hakika haikubari aliongeza,

Lowasa Tafuta Chama, CCM kimekushinda aliongeza Katibu huyo
KATIBU WA VIJANA TAIFA AKIFAFANUA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI,

No comments