Zinazobamba

JINSI TGNP WALIVYOUPINGA UKATILI WA KIJINSIA, WASEMA RASILIMALI LAZIMA ZIELEKEZWE HUKO ILI KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA

Mtandao wa kijinsia Tanzania  lumeitaka serikali kuelekeza rasilimali katika nyanja ya ukatili wa kijinsia kama kweli taifa limejizatiti kutaka kutokomeza ukatili wa kijinsia hapa nchini,

Tamko hilo limetolewa mapema hii leo wakatika mkutano wa maadhimisho ya siku 16 za  kupinga ukatili wa kijinsia  hapa nchni uliofanyika mapema hii leo, katika viwanja vya TGNP vilivypo maeneo ya mabibo,

Akizungumzia hali halisi ya ukatili wa kijinsia,mwakilishi wa TGNP taifa, Bi. Mary Nsemwa amesema kuwa ukatili wa kijinsia bado ni janga la kitaifa , na kwamba hatua za haraka zinahitajika ili kutokomeza kabisa janga hili ambalo linaota miziz kila kukicha, Nsemwa amesema, ili kuondoa tatizo hilo kwa sasa, Serikali haina budi ielekeze rasilimali za kutosha katika tatizo hilo,

MWAKILISHI WA JESHI LA POSI MAKAO MAKUU, CPL KURUTHUM AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA WADAU WA KIJINSIA KATIKA VIWANJA VYA TGNP
Naye mwakilishi wa polisi tokea toka makao makuu, D/CPL KURUTHUM MIKIDADI, amesema kwa upande wao jeshi la polisi wamejipanga sawia kukabiliana na changamoto za ukatili wa kijinsia na kwamba kwa kuanzia tayari wameunda dawati la kijisia katika ofisi hizo za jeshi ambazo zinahudumia kesi za kijinsia,

CPL Kuruthum amendelea kusema kuwa, Madawati ambayo yameunda katika ofisi za jeshi la polisi zitasaidia sana kutatua kero za kijinsia ambazo hapo awali zilikuwa hazipatiwi ufumbuzi,
Amewataka wananchi kuzitumia ipasavyo madawati hayo, na kwamba wataalam wa kutosha wapo wa kujadili mambo ya kijinsia ,wasiogope waje ili wapatiwe ufumbuzi wa matatizo yao ya kijinsia hata kama ni ya faraghaa

WADAU WA JINSIA WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI AFISA WA JESHI LA POLISI AKITANGAZA  UMUHIMU WA DAWATI LA JINSIA KATIKA OFISI ZA JESHI  HILO, KURUTHUM ALIWATAKA WANANCHI KUTUMIA FULSA KWA KUPELEKA KERO ZAO ILI WAPATIWE HAKI ZAO


TUNASIKILIZA, WADAU WAKIFUATILIA KWA MAKINI

ULINZI SHIRIKISHI NAO  HAWAKUWA MBALI KATIKA HARAKATI ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA, ASKALI HAO AMBAO WAPO NDANI YA JAMII WALILIOMBA JESHI LA POLISI KUWAPA KAZI YA KWENDA KUTOA ELIMU VIJIJINI JUU YA UKATILI WA KIJINSIA ILI WAKAZI WA VIJIJINI WAWEZE KUPAZA SAUTI ZAO, HATA HIVYO OMBI HILO LIMECHUKULIWA NA LITAWASILISHWA SEHEMU INAYOTAKIWA





MMOJA WA WADAU WALIOHUDHULIA KATIKA MAADHIMIASHO HAYO YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA, BI. HUYU ALIKUWA AKIWAKILISHA KUNDI MAALUM YA WALEMAVU, AMESEMA WALEMAVU NAO WATU WASINYANYASE KWA KUJAZWA MIMBA HOVYO KISHA KUWAKIMBIA NA KUFANYA OMBAOMBA WAWE WENGI HAPA NCHINI

No comments