Unyama: Watanzania wawili wapigwa na POLISI wa Mabibo wakiwamahabusu na kuvunjwa miguu na mikono
Askari polisi wa Kituo Kidogo cha Polisi cha Mabibo,
wanatuhumiwa kwa kuwapiga na kuwavunja miguu na mikono, wakazi wawili wa eneo
la Jitegemee.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 17 mwaka huu saa 5 usiku wakati
wakazi hao,Maulid Yahaya na Willium Six, wakiwa wanakunywa vinywaji
kwenye duka
lililopo eneo la Mabibo Mwisho.
Habari zilisema wakati watu hao wakijiburudisha, alijitokeza mtu mmoja na kuaanza kuwafanyia fujo jambo lililosababisha wote wawili kupelekwa kwenye Kituo Kidogo cha Polisi Mabibo.
Akizungumzia tukio hilo, Yahaya alisema wakati tukio hilo
likiendelea kufanyika, mtu huyo alichukua filimbi na kuanza kuipiga
ndipo walijitokeza watu na kuwapeleka kwenye kituo hicho.
Alisema walipofikishwa kituoni, ilitolewa amri na polisi
kuwa wapigwe kabla ya kuingizwa mahabusu ndipo alipojitokeza askari
polisi mwingine akiwa na mgambo ambao walianza kuwashambulia kwa kutumia
visu na virungu huku wakiwa wamefungwa pingu.
Alisema ilipofika saa 9 usiku walifuatwa na gari la polisi
na
kuhamishiwa kwenye Kituo cha Polisi cha Urafiki ambako
walikaa mahabusu siku mbili bila ya kupelekwa hospitali.
Yahaya alisema wakiwa mahabusu waliwaomba askari polisi, ili
waweze kupelekwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa huduma kutokana
na majeraha waliokuwa wameyapata.
"Tunataka kujua sheria ipi inamruhusu askari polisi
kumpiga raia akiwa mahabusu bila ya kusikiliza maelezo yake,” alisema Yahaya.
Kwa upande wake, Six alisema Oktoba 19 mwaka huu saa 8
mchana waliruhusiwa kutoka kituoni baada kesi yao kufutwa na mtu
aliyewafanyia fujo wakati wanakunywa vinywaji.
Alisema baadaye walimfuata mmoja wa askari na kumweleza kuwa
walipigwa na askari wa Kituo Kidogo cha Polisi Mabibo lakini alikataa
kuchukua maelezo yao.
Six alisema walipelekwa Kituo cha Afya cha Sinza ambako
walipigwa picha ya X-ray na kugundulika kuwa mguu wake wa kushoto umevunjika
mara mbili huku Yahaya akiwa amevunjika mkono.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura,
alisema hajata taarifa na kwamba anafuatilia.
-Mwananchi and mpekuzi
No comments
Post a Comment