Hivi ni vyuo 10 vya Tanzania vilivyofutwa na Serikali......chunga sana usije ukaingia mkenge
SERIKALI
kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imevifuta vyuo 10 ambavyo
havikusajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) . Naibu Waziri wa
wizara hiyo, Philip Mulugo, alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaama mbele ya
Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na kuongeza kuwa kufutwa kwa vyuo hivyo ni
kutokana na kutokufuata utaratibu wa kusajiliwa.
Alivitaja vyuo hivyo ni Media
and Research Center, Vision Hotel and Tourism College, East Africa College of
Hospitality and Tourism, The Africa Institute of Business Management na Aspiration
Training Center, vyote vya Dar es Salaam.
Vingine ni Dar es Salaam School of
Hair Design, Media and Values Training Institute na Information Technology
Training Center vya Dar es Salaam.
Pia alikitaja Chuo cha Morogoro School of
Medical Sciences cha Morogoro. Katika hatua nyingine, Mulugo alikiri kuwa kuna
upungufu katika kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia bodi ya
mikopo.
Alisema kuna changamoto nyingi zinazoikabili bodi hiyo zikiwamo
urejeshwaji wa mikopo kwa wanafunzi waliomaliza chuo, mfumo wa utoaji wa
mikopo, ufinyu wa bajeti na makosa yanayotokana na wanafunzi kukosea kujaza
fomu za mikopo.
No comments
Post a Comment