Zinazobamba

TBS SASA YAMULIKA NGUO ZA NDANI ZA MITUMBA, YASEMA ATAKAYEBAINIKA KUUZA BIDHAA HIYO KUKIONA,


Shilika la viwango tanzania limetangaza msako mkali huko masokoni ili kuweza kuwabaini wale wote waliokataa agizo halali la shilika hilo la kutouza bidhaa ya nguo za ndani katika masoko ya hapa nchini, 
AFISA UHUSIANO WA SHILIKA LA VIWANGO TANZANIA  (TBS) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari, roida amesema katika zoezi hilo hawana utani na ni kwamba watakaokamatwa na nguo hizo za ndani, nguo zao zitateketezwa na muhusika kuchukuliwa hatua

Akizungumza na wanahabari hivi karibuni jijini daresalam, afisa uhusiano wa shirika hilo bi Roida, amebainisha kuwa uuzaji wa nguo za ndani za mitumba katika masoko yetu hairuhusi kisheria na kwamba tayari wameshafanya matangazo mbalimbali kuwataarifu wafanyabiashara wa nguo hizo lakini bado wameonekana kuendelea kukaidi maagizo ya shilika,

Amesema wameamua kuanzisha msako huo kwa kila soko na kwamba watambatana na askari polisi pamoja na mgambo wa jiji katika operesheni hiyo itakayoanza katikati ya wiki hii katika masoko ya jiji la daresalaam

ameendelea kusema kuwa kwa mujibu wa sheria namba mbili ya mwaka 2009, nguo za ndani za mitumba haziruhusiwi na kwamba ikibainika wafanyabiashara wanaendelea kuziuuzwa, nguo hizo zitateketezwa na muhusika kuchukuliwa hatua za kinidhamu

No comments