Zinazobamba

MAHAKAMA ZA TANZANIA KUANZA KUTUMIA TEHAMA, NI BAADA YA KUBORESHEWA BAJETI YAO TOKA BILION 30 MWAKA 2012/13HADI KUFIKIA BILIONI 140 MWAKA 2013/14


MAHAKAMA ya tanzania imedhamilia kuanza kutumia matumizi ya tehama katika mahakama zakekuanzia ngazi ya mahakama ya rufani hadi za wilaya ili kurahisisha kutunza kumbukumbu za mashauli yanayotolewa hukumu katika mahaka zetu na kumrahishia mdau kupata hukumu zake kwa nzia ya mtandao
Msajiri mwandamizi wa mahakama ya Tanzania akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari, masijiri huyo amesema sasa matya tehama yataanza rasmi katika mahakama zetu


Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jiji daresalaam, Naibu msajiri mwandamizi wa mahakama kuu ya Tanzania Bw.John Kahyoza amesema sasa wamejipanga kuhakikisha kuwa matumizi ya tehama katika mahakama zetu zinaimalika na kwamba tayari mchakato uko katika njia sahihi, 

ameongeza kusema kuwa awali matumizi ya tehama katika mahakama zetu zilikua ni kitendawili kutokana na ukweli kuwa miundo mbinu ya majengo yetu si rafiki kwa kuweka kompyuta na kuendelea kutumika vizuri pili bajeti nayo ilikuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya tehama katika mahakama zetu,,

Wataalamu wa mifumo ya mitandao nao walikuwa kuwapata ni tatizo kutokana na wataalamu wengi kutaka kuajiriwa mjini na sio katika mawilaya zetu, sasa kwa bajeti hii tunaweza kutimilza malengo aliongeza , msajiri huyo mwandamizi wa mahakama ya Tanzania
Aidaha katika hatua nyingine, msajiri huyo aekiri kuwa bado wataendelea kutumia lugha ya kingereza kama lugha ya kuwekea kumbukumbu katika mahakama zetu za rufaa na mahakma kuu ili kutoifanya mahakama zetu kuwa kama kisiwa ambacho huwezi kubadilishana ujuzi na mahakama zingine za kimataifa,

Amesema kwa mahakama zetu za mwanzo bado lugha za mawasiliano itabaki kuwa kiswahili na kwamba hata kumbukumbu itahifadhiwa katika lugha hiyo, ili kurahisisha mawasiliano kati ya mlalamika na mlalamikiwa
wanahabari wakiwa kazini


No comments