TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI VYA SADC.JK MGENI RASMI
MKURUGENZI WA TBC NDG CLEMENT MSHANA PAMOJANA VIONGOZI WENGINE WA SHIRIKAHILO WAKIZUNGUMZIA MKUTANO HUO |
Tanzania imepata nafasi ya kuwa
mwenyeji wa mnkutano mkubwa wa mwaka wa vyombo vya habari vya utangazaji
vya nchi za jumuiya ya maendeleo kusini mwa africa.mkutano huo ambao
umeandaliwa na chama cha vyombo vya utangazaji vya nchi hizo SOURTHEN
AFRICA BROADCASTING ASSOCIATION au kwa kifupi SABA unatarajiwa kufanyika
jijini arusha tarehe 21 hadi 24 mwezi wa kumi mwaka huu katika ukumbi
wa AICC jjini arusha
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam mkurugenzi wa TBC CLEMENT MSHANA amesema kuwa mkutanohuo unatarajiwa kufunguliwarasmi na raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania MH JAKAYA MRISHO KIKWETE huku viongozi wengine wengi kama waziri wa habari,vijana utamaduni na michezo,waziri wa maliasili na utalii pamoja na mawasiliano sayansi na technologia wakitarajiwa kuwepo.
Katika mkutano mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemotechnologia ya digit na changamoto zake huku kauli mbiu ya mkutano huo ikiwa ni NAFASI YA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUKUZA UTALII
No comments
Post a Comment