Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava (kushito) akisalimiana na Mike Bess ambaye ni mshauri na mmoja wa waanzilishi wa Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia mazingira na nishati jadilifu (CAMCO) wakati wa warsha ya siku moja ya kujadili uandaaji mkakati wa nishati – tungamotaka (Biomass) nchini inayofanyika leo katika Hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava akiongea na washiriki wa warsha ya siku moja ya kujadili uandaaji mkakati wa nishati – tungamotaka (Biomass) nchini inayofanyika leo katika Hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia mazingira na nishati jadilifu nchini (CAMCO) Jett Felten na kushoto ni mhadhili wa Chuo kikuu cha Sokoine (SUA) ambaye pia ni mshauri wa CAMCO Prof. Romanus Ishengoma. Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava akiongea na washiriki wa warsha ya kujadili uandaaji mkakati wa nishati – tungamotaka (Biomass) nchini inayofanyika leo katika Hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo ya siku moja imeandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia mazingira na nishati jadilifu nchini (CAMCO). Washiriki wa warsha ya siku moja ya kujadili uandaaji mkakati wa nishati – tungamotaka (Biomass) nchini wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava (hayupo pichani) wakati akifungua warsha ya siku moja ya kujadili uandaaji mkakati wa nishati – tungamotaka (Biomass) nchini leo katika Hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam. Hivi sasa Serikali iko katika mchakato wa kubadilisha sera ya nishati ili iweze kutekeleza mkakati wa tungamotaka. Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava (kushoto) akiongea jambo na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia mazingira na nishati jadilifu nchini (CAMCO) Jett Felten mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa warsha ya siku moja ya kujadili uandaaji mkakati wa nishati – tungamotaka (Biomass) nchini inayofanyika leo katika Hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam. Washiriki wa warsha ya siku moja ya kujadili uandaaji mkakati wa nishati – tungamotaka (Biomass) nchini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa kwa warsha hiyo leo katika Hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam. Hivi sasa Serikali iko katika mchakato wa kubadilisha sera ya nishati ili iweze kutekeleza mkakati wa tungamotaka. Picha na Anna Nkinda – Maelezo
No comments
Post a Comment