Zinazobamba

KOVA AWAPIGA STOP CHADEMA,CUF NA NCCR, WALITAKA KUFANYA MAANDANO YA KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA KATIBA, ATAJA SABABU ZA KUWAZUIA

KAMISHINA wa polisi kanda maalum ya Daresalam, Kamishina Suleimani Kova amepiga stop maandamano yaliyotaka kuendeshwa na vyama vya upinzani vilivyoungana hivi karibuni yakiwa na lengo la kuhamasisha wananchi wa jiji la daresalaam kushiriki katika mchakato unaoendelea sasa wa katiba mpya
KOVA AKIFAFANUA JAMBO KWA WAANDISHI WA HABARI

Akizungumza na waandihsi wa habari ofisini kwake Kamishina kova amesema Chama cha Chadema,Cuf na Nccr waliwaandikia jeshi la polisi barua ya kutaka kufanya maandano siku ya jumamosi yatakayoanzia huko maeneo ya tazara yakipitia njia ya uhuru road mpaka kariako eneo la faya na kumalizikia pale jangwani

Amesema baada ya kupokea barua hiyo wameangalia viashiria vyote vya usalama na kugundua kuwa usalama wa raia ungekuwa hatarini na pia ungsababisha shughuli mbalimbali kusimama kwa siku hiyo hivyo wameamua kusitisha maandamano hayo na badala yake wameruhusu kuendelea kwa mkutano wa hadhara utakaofanywa na muunganiko wa vyama hivyo katika viwanja vya jangwani

Amesema tayari wameshakaa na viongozi wandamizi wa vyama hivyo akiwemo naibu katibu mkuuu wa CUF Bw Jurius Mtatiro, na katibu mkuu wa vijana wa chadema Bw. John Henje na kukubaliana masuala muhimu kwa faida ya watanzania wote,
KOVA AKIFAFANUA KWA WAANDISHI WA HABARI

Maandamano yangesababisha Foleni isiyokuwa ya lazima, kuleta usumbufu kwa wananchi wengine ambao wangetaka kufanya shughuli zao za kujenga taifa, kuruhusu maandamano hayo ni sawa na kusema siku nzima wananchi walale nyumbani alisema kamishina kova

No comments