VIJANA TUMIENI UMOJA WENU KUSHAWISHI WAJUMBE WENU WA BALAZA LA KATIBA, NI KATIKA KUYAINGIZA MAMBO MUHIMU YOTE YA VIJANA- MEYA
Na Selemani Ahamadi
Vijana wametakiwa kuhakikisha kuwa mambo yao muhimu
yanajumuishwa katika katiba inayoendwa kuundwa kwa kutoa ushawishi wa vitu
wanavyotaka viwemo katika katiba hiyo kwa wajumbe wao wa balaza la katiba ili
mambo hayo yaweze kutetewa kwa nguvu zote katika mabalaza ya katiba
| MEYA WA MANISPAA YA ILALA MH. JERRY SLAA AKIFAFANUA JAMBO KWA VIJANA WALIOHUDHURIA KONGAMANO LA KUJADILI RASIMU YA KATIBA JIJINI DARESALAAM |
Wito huo umetolewa na meya wa manispaa ya Ilala Bw. Jerry
Slaa wakati akitoa mada kwa vijana wapatao 120 toka wilaya 50 za Tanzania bara
na visiwani katika kongamano la vijana lililofanyika mapema hii leo jijini
Daresalaam
“Haki kama ya kijana kuchaguliwa kuwa mbunge rasimu inasema
ni lazima afike umri wa miaka 25 wakati umri wa jumla kwa mwananchi kuruhusiwa
kupiga kura ni kuanzia miaka 18, hii inamaanisha kuwa kijana mwenye umri wa
miaka 18hadi 24 hana haki ya kuchaguliwa kuwa mbunge wakati huo huo ana haki ya
kuchagua mbunge wake hii sio haki hata kidogo” aliongeza Bw. Slaa
Amesema kuna watu vijana lakini wamefanya mambo makubwa
kabisa na pia wapo watu wazima wameshindwa kufanya kazi nzuri kama ya
kijana,hivyo kudhani kuwa kijana hawezi kufanya kazi nzuri si kweli kwani
vijana wanaweza
| BAADHI YA VIJANA WALIOHUDHURIA KATIKA KONGAMANO HILO WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI MH JERRY SILAA |
Aidha katika hatua nyingine Slaa amewataka vijana naviongozi
wa ngazi mbalimbali kuiangalia katiba kwa maslahi ya taifa letu na wala wasiweke
maslahi ya chama ama taasisis yeyote kwani chama kinapita lakini taifa lipo
vizazi na vizazi
“Hata unapoenda kuwashawishi wajumbe wenu wa balaza la
katiba hakikisheni mnashawishi mambo ambayo yana masilahi kwa taifa,kwani
kufanya hivyo kutasaidia kuingiza masuala muhimu ya kulijenga taifa letu “amesema
Bwana Slaa
Akitolea mfano wa maeneo ambayo vijana hawana budi
kuyaangalia ni pamoja na maeneo ya elimu, haki za kupiga kula ambazo kwa kiasi
fulani zimeonyesha udhaifu katika rasimu ya katiba ambayo inaenda kuchambuliwa
katika mabalaza ya katiba
| KAIMUMKURUGENZI WA TYC NDUGU LENIN KAZOBA AKIFAFANUA JAMBO KWA WAANDISHI WA HABARI |
Naye kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa Taasisis ya vijana
Tanzania Youth Coalition (TYC) Bw. Lenin
Kazoba ambayo ndio walioandaa kongamano hilo, amewataka vijana
kushikamana pamoja ili sauti zaoili ziweze kusikika katika katiba mpya
Kongamano hilo ambalo limeandaliwa mahususi kabisa kwa lengo
la kuwapa fulsa vijana kutathmini mchakato wa kutengeneza katiba, kujadili
rasimu ya katiba limelenga kutoa maoni ya vijana ambayo yatawasilishwa kwenye
tume ya mabadiliko ya katiba na wadau wengine wa maendeleo ili yaweze
kusikilizwa na kuingizwa katika katiba mpya
MWISHO
No comments
Post a Comment