Tanesco yaanzisha kitengo cha kushughulikiawateja wake wakubwa,CTI wasema ni wakati muafaka
Kampuni ya TANESCO imewahakikishia shirikisho la viwanda na
wafanyabiashara CTI kuwapatia umeme wa uhakika na kwamba kwa kuanzia
wameanzisha idara itakayoshughulika na wanachama wa shilikisho hilo moja kwa moja kutatua kero zao
zinazowakabili
Akizungumza katika mkutano maalum uliowashirikisha wanachama
wa shirikisho hilo la CTI na uongozi wa kampuni ya Tanesco mapema hii leo,
Mkurugenzi mtendaji wa Tanesco Eng Felchesmi Mramba amesema hatua ya kuwa na
kitengo cha huduma kwa wateja wanaotumia kwa kiasi kikubwa umeme wa Tanesco
umefikiwa ili kuweza kuwa karibu na watumiaji hao na wao pia kuweza kutoa kero
zao kwa muda muafaka na kupatiwa ufumbuzi wa haraka
| KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO eNG. FELCHESMI MRAMBA AKIFAFANUA JAMBO KUHUSU UHAKIKA WA UMEME KATIKA JIJI LA DARESALAAM |
Eng Mramba ameendelea kusema kuwa kwa sasa wamiliki wa
viwanda, na wafanyabiashara wakubwa wamekuwa wakitumia takribani asilimia 60 ya
umeme wote unaodhalishwa na Tanesco hivyo ili kuweza kuwajali na kusikia kero
zao kwa karibu tumeamua kuweka kitengo hicho ambacho tunaamini kitasaidia kwa
kiasi kikubwa kupunguza kero ambazo walikuwa wanakumbana nazo
“Tunaamini kwa ushirikiano tutakaouonyesha utaweza
kuwawezesha wamiliki wa viwanda na wafanyabiashara wakubwa kuongeza uzalishaji
wao kwa kiasi kikubwa na hivyo kuweza kuinua uchumi wa taifa letu” aliongeza
Eng Mramab
| Eng. MRAMBA AKIFUATILIA MOJA YA MAWASILISHO YA MIRADI MBALIMBALI INAFANYIWA KAZI NA KAMPUNI YAKE,WADAU WA CTI WALIPATA FULSA YA KUSIKILIZA MIRADI HIYO NA KUTEMBELEA BAADHI YA JIJI LA DARESALAAM |
Aidha katika hatua nyingine Eng Mramba amebainisha miradi
mbalimbali ambayo inatekelezwa na ile ambayo bado haijaanza rasmi kutekelezwa
hiyo ikiwa ni jitihada za kuwahakikishia wanachama hao wa CTI kuona ni jinsi
gain Kampuni imejipanga kuwepo kwa umeme wa kuaminika hapa nchini na kuwapa
wanachama hao fulsa ya kujipanga namna gain wanaweza kuongeza uzarishaji wa
bidhaa zao,
Miongoni mwa miradi iliyowasilishwa kwa wamiliki hao wa
viwanda ni pamoja na ile miradi ya kujenga vituo vyenye megawati kubwa ya pale
Ubungo,Kurasini Gongo la mboto na Kinyerezi ambapo ikimalizika hakutakuwa na
tatizo la umeme kabisa katika jiji la Daresalaam
| MWENYEKITI WA SHIRIKISHO LA VIWANDA NA BIASHARA CTI AKIFAFANUA JAMBO KWA WANACHAMA WA CHAMA HICHO MAPEMA HII LEO KATIKA OFISI ZA TANESCO |
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa shirikisho la viwanda na
wafanyabiashara CTI BW. Felex Mosha amepongeza hatua zilizochukuliwa na uongozi
wa Tanesco kwa kuandaa idara itakayoshughulika moja kwa moja na wanachama wake
kwani hatua hiyo inategemewa kuongeza tija kwa wafanyabishara na wamiliki wa
viwanda kwa kupatiwa umeme wa uhakika
| MMOJA WA WANACHAMA WA CTI AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA MKURUGENZI WA TANESCO MAPEMA HII LEO |
Aidha Bw. Mosha amepongezajuhudi za kuwaleta pamoja wadau wa
umeme na kukaa meza moja kuzungumzia pamoja kero za umeme katika viwanda vyetu
na kwamba kuanzia sasa sisi kama
wamiliki wa viwanda tutakuwa katika nafasi nzuri ya kujua kinachoendelea katika
suala zima la umeme na kuwataka viongozi hao wasiishie kuwaita tu katika
mikutano na badala yake watoe taarifa za umeme kwa haraka zaidi ili waweze
kuchukua tahadhari mapema
“Tunawomba nyinyi kama
tanesco kutupatia taarifa ya katizo la umeme mapema iwezekanavyo ili tuweze
k
| MDAU AKIMAKINIKA KUFUATILIA MADA ZINAZOENDELEA |
| HAPA WADAU WA CTI WAKIONYESHA MOJA YA VITUO VYA KISASA CHA UBUNGO AMBACHO KITASAIDIA KUPUNGUZA TATIZO LA UMEME HAPA JIJINI, KINADHALISHA JUMLA YA KW 180 |
| CTI WAKIWA WANAANGALIA MITAMBO YA KUZALISHA UMEME WA UHAKIKA |
ujiandaa, na tunaamini kwa sababu ninyi ni sura mpya basi hata matendo yenu
yatakuwa mapya na ndio maana hata leo tumeanza ushirikiano mpya na nynyi”
aliongeza Bw Mosha
Wamiliki hao pia wamepata fulsa ya kujionea miradi
mbalimbali inayoendelea katika jiji la Daresalaam
No comments
Post a Comment