TAARIFA YA KIKWETE KUZINDUA CHAMA CHA WAZAZI WENYE WATOTOTO WALEMAVU WA MTINDIO WA UBONGO AKILI NA VIUNGO TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UZINDUZI
WA CHAMA CHA WAZAZI WA WATOTO WENYE ULEMAVU WA MTINDIO WA UBONGO, AKILI NA
VIUNGO TANZANIA. (CHAWAUMAVITA)
UTAKAOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI AGOSTI 24’ 2013 KATIKA UKUMBI WA SABASABA AMBAPO
MGENI RASMI ANATARAJIWA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA
JAKAYA MRISHO KIKWETE.
1.0 UTANGULIZI
Kwa kuwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za Binadamu
kwa watoto wenye ulemavu wa Mtindio wa ubongo, akili na viungo vimekuwa
vikishamiri nchini;
Na kwa kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa wakifarakana,
kukimbiana, na hata kumtelekeza mtoto na pia wakati mwingine kumdhuru mtoto
mwenye ulemavu baada ya mtoto huyo kuzaliwa au kupatwa na ulemavu baadaye;
Na kwa kuwa kumekuwa na dhana potofu iliyotawala
katika jamii juu ya upatikanaji wa watoto wenye ulemavu wa mtindio wa ubongo, akili
na viungo na maisha yao kwa ujumla;
Na kwa kuwa hakuna huduma za awali kabla na baada ya
tatizo zilizo endelevu zitolewazo kwa watoto wenye mtindio wa ubongo, akili na
Viungo kwa watoto/watu wanoishi na ulemavu huo;
Na kwa kuwa mipango na mikakati iliyopo nchini haikidhi changamoto
zinazoendelea kujitokeza kwa
watoto/watu wenye ulemavu wa mtindio wa ubongo, akili na viungo nchini;
Na kwa kuwa
mtoto mwenye ulemavu ni sawa na mtoto mwingine yeyote anastahili kupata
huduma na vifaa tiba maalum vya matibabu, na nafasi sawa ya elimu na mazoezi
ili kumsaidia kufikia malengo yake ya kimaisha;
Na kwa kuwa sisi wazazi na wananchi kwa ujumla tuna
jukumu la awali la kuhakikisha kuwa
watoto/watu wenye ulemavu wa mtindio wa
Ubongo na Viungo wanakuwa salama na duniani panakuwa ni mahala bora pa kuishi
kwao;
HIVYO
BASI Sisi Wazazi wa Watoto wenye Ulemavu wa Mtindio wa
Ubongo na Viungo tunaopata huduma katika Hospitali na vituo vya CCBRT tuliamua, kuunda chama kiitwacho CHAMA CHA WAZAZI WA WATOTO WENYE ULEMAVU WA
MTINDIO WA UBONGO, AKILI NA VIUNGO TANZANIA. (CHAWAUMAVITA)
Dira ya CHAWAUMAVITA ni kuwa CHAMA cha mfano
kinachochangia upatikanaji wa huduma
bora na endelevu kwa watoto wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo
Tanzania ili kuhakikisha watoto wenye Ulemavu huo wanasaidiwa kukabiliana na
changamoto zilizopo na kuandaa mazingira bora ya makuzi na maisha yao kwa
ujumla.
Chama kimesajiliwa na Wizara ya Mambo ya ndani tangu
March 19, 2013 kwa usajili wenye namba S.A 18732.
2.0
MALENGO YA CHAWAUMAVITA NI:-
Kuwaleta pamoja watu/familia zinazolea watoto wenye ulemavu wa mtindio wa Ubongo, akili
na viungo ili kubadilishana uzoefu, kupata elimu ya namna ya kuwatunza watoto
wenye ulemavu huo.
Kutoa elimu ya ulemavu wa Mtindio wa Ubongo na
Viungo kwa jamii ili Kupunguza athari na
maumivu yatokanayo na Mtindio wa Ubongo, akili na viungo.
Kukusanya, kuchapisha na kusambaza taarifa
zinazohusu matatizo yatokanayo na ulemavu wa Mtindio wa Ubongo,akili na viungo.
Kuwasaidia wanachama/wazazi katika kuwatunza na kutetea na kupata haki zao kwa mujibu wa
sheria.
Kujenga na kuendeleza vituo vya mazoezi tiba, kuratibu
na kusambaza vifaa tiba kwenya vituo na;
Kujenga na kuimarisha vituo kwa ajili ya masuala ya
kijamii na michezo kwa watoto wenye
ulemavu
3.0
MAFANIKIO
Kwa takribani kipindi cha mwaka mmoja tangu
kuanzishwa na kusajiliwa kwa chama, tumeweza kufanya yafuatayo;
·
Kujenga
mawasiliano mazuri na taasisi za serikali ,binafsi na za kiraia.
·
Mwaka jana
kupitia wizara ya afya,tuliweza kupata mfadhili kampuni ya Montero minning
and exploration kwa kushirikiana na taasisi ya EOTF ya mama ANNA
MKAPA ambapo watoto walemavu 50 waliweza kupatiwa baiskeli za watoto wenye
ulemavu kutoka katika vituo mbali mbali jiji Dar es salaam.
·
Kupata usajili
wa kamili,kuandikisha wanachama wapya na kuongeza hamasa kwa wazazi wenye
watoto walemavu.
4.0
CHANGAMOTO
·
ELIMU kuhusu
upatikanaji wa watoto wenye ulemavu haijafikishwa kwa jamii vya kutosha,
·
Elimu juu ya
utunzaji, mazoezi tiba, huduma za kijamii juu ya watoto walemavu kwa wazazi
imekuwa hairidhishi
·
Asilimia kubwa
ya wazazi wenye watoto walemavu ni akina mama wa nyumbani ambao hawana fursa ya
kupata bima za afya hivyo utunzaji wa watoto
ni gharama kubwa.
·
Kina mama
kukimbiwa na wenzi wao kutokana na kuwepo kwa mtoto mwenye ulemavu.
·
Gharama kubwa
za huduma za matibabu kwa watoto wenye ulemavu .
·
Uchache na
umbali na maeneo yasiyo rafiki katika vituo vya mazoezi tiba kwa watoto wenye
ulemavu,
·
Uchache wa
watoa huduma ya mazoezi tiba katika vituo vya mazoezi tiba
·
Uhaba wa dawa
katika vituo vya afya ambapo kwa mujibu wa sera ni bure kwa watoto.
5.0
UZINDUZI
Baada ya Usajili, CHAWAUMAVITA inaandaa Mpango
Mkakati wa Miaka mitano 2013-2018 ambao una
lengo la kuwasaidia watoto wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo akili na
Viungo pamoja na kutoa elimu kwa jamii ili kwanza jamii ishiriki katika kuzuia
upatikanaji wa watoto hawa na pia iwalee na kuwasaidia kupata mahitaji yao
muhimu ya kila siku pamoja na kufikia malengo yao ya kimaisha
Ni
kwa muktadha huu Ndio maana tumeamua kufanya Uzinduzi wa Chama cha CHAWAUMAVITA
tumetuma maombi kwa mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mgeni rasmi ili:-
Ø Kuishirikisha jamii na wadau wengine kushiriki
katika harakati kupigania ustawi wa watoto wenye ulemavu kwa maslahi ya watoto
wote wa Tanzania wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo.
Ø Kuzindua Mpango Mkakati wa chama wa miaka mitano
2013-2018.
Ø Kuonyesha Makala Filamu (Documentary) inayoonyesha
hali halisi ya maisha ya jamii inayowalea watoto wenye ulemavu wa Mtindio wa
Ubongo Akili na Viungo pamoja na walezi wao.
Ø Kuzindua tovuti ya Chama na kualika juhudi za wadau
katika kuchangia harakati za kufikia malengo ya Chama na jamii kwa ujumla.
Uzinduzi utafanyika siku ya jumamosi ya tarehe
24.08.2013, saa 4:00 Asubuhi hadi saa 8:00 Mchana. Na Mgeni rasmi anatarajiwa
kuwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr Jakaya Mrisho Kikwete.
Chawaumavita
inachukua fursa hii kuwaalika wadau wote muhimu wakiwemo waandishi wa habari,
Serikali, Mabalozi, Asasi na taasisi mbalimbali sio tu kushiriki bali kuchangia
katika kufanikisha katika tukio hili muhimu la kihistoria kwa maslahi
ya watoto wenye ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na viungo Tanzania.
Imtolewa na
.............................................
Jonathan Kawamala
MWENYEKITI
CHAWAUMAVITA
Tunaamini-
“Umoja daima ndio suluhisho kwa changamoto”
Kwa
pamoja tukishikamana tutashinda.
AHSANTE kwa kunisikiliza!
No comments
Post a Comment