Zinazobamba

TUMEZITAMBUA RASMI BLOGS, SASA ANDIKENI MAZURI NA SI KUCHAFUANA, NKOMA

MKURUGENZI WA TCRA PROF. JOHN NKOMA AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA MKUTANO WA WADAU WA MAWASILIANO,
 TCRA SASA YAANZA KUZITAMBUA BLOGS, WADAU WASEMA NI HATUA NZURI KWA SERIKALI KUZITAMBUA
Kufuatia ukuaji wa  watumiaji wa mitandao kuongezeka kila kukicha huku wamili wa mitandao ya kijamii wakiendelea kuongezeka kila leo, malaka ya  mawasiliano Tanzania Imeamua kuwatambua rasmi wamiliki wa mitandao hiyo ya kijamii kuwa ni moja ya vyombo vya kuaminika kwa kutoa taarifa za kuelimisha, kuburudisha na kuonya wananchi


Akizungumza katika kampeni maarum ya kuhamasisha matumizi mazuri ya mawasiliano kwa wananchi, mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya mawsilano TCRA Bw. Amesema wameamua kuwatambua rasmi mitandao ya kijamii  kama inamchango mkubwa sana wa kuujulisha umma habari mbalimbali zinazoendelea ndani na nje ya nchi

Mkurugenzi huyo ameendelea kusema kuwa kwa sasa kuna idadi kubwa ya watumiaji wa mitandao ambapo mpaka sasa jumla ya wananchi wapatao milioni 7.6 wanaendelea kupata taarifa kupitia njia ya mitandao ukilinganisha na idadi ya wananchi laki tatu ambao walikuwa wakitembelea mitandao kwa kipindi cha miaka mitau iliyopita
 IMG_1643  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Bw. Profesa John Nkoma  akimsikiliza Msanii Mrisho Mpoto wakati alipokuwa akitoa ujumbe wake kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha matuzimizi mazuri ya mitandao ya mawasiliano uliofanyika katika makao makuu ya mamlaka hiyo Sinza barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es salaam leo.                                                                                      
Hata hivyo mkurugenzi huyo amewataka wadau wa Blogs hapa nchini kuacha tabia ya kuandika mambo ambayo yanasababisha uvunjifu wa amani au udhalilishaji kupitia BLOGS hizo kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria ya mawasiliano ya kielectroni na posta (EPOCA) mwaka 2010
“watanzania walio wengi sasa wanafaidika na huduma za mawasiliano kupitia blog zenu hivyo ni vema mkaandika vitu vya ukweli kwani ukweli utawafanya wateja wenu wakubwa wanaotembelea blog zetu kupata vitu ambavyo si vya kubabaisha na hivyo kuweza kujijengea heshima kwa wananchi unaowahudumia ” aliongeza Bw…

Naye mmoja wa wamiliki wa Blogs maarufu hapa nchini Bw. Othmani Michuzi ameisifu serikali kwa hatua waliochukua ya kuitambua rasmi mchango wa wanablog hapa nchini na kuahidi kuwa watahakikisha wanafuata maadili yote ya uandishi wa habari ili kuweza kuwapa wananchi vitu vya uhakika na kwa wakati

Kwa sasav Blogs zinatoa Taarifa kwa haraka zaidi ukilinganisha na midia zingine nah ii ni kutokana na ukweli kuwa waendesha BLOGS wote wanahakikisha taarifa zao zinawafikia wateja wao kwa wakati
MMOJA WA WAMILIKI W A BLOG BW. OTHMANI MICHUZI AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI

 
IMG_1643
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Bw. Profesa John Nkoma  akimsikiliza Msanii Mrisho Mpoto wakati alipokuwa akitoa ujumbe wake kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha matuzimizi mazuri ya mitandao ya mawasiliano uliofanyika katika makao makuu ya mamlaka hiyo Sinza barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es salaam leo. Katika uzinduzi huo TCRA imesema kwa sasa inatambua rasmi mitandao ya kijamii kama blogs kwamba ni vyombo kamili vya habari na kwamba kwa sasa mamlaka hiyo inaadaa utaratibu wa kukutana na bloggers na kuzungumza nao juu ya matumizi mzuri ya mitandao na kutafuta wataalamu kwa ajili ya kutoa mafunzo mbalimbali juu ya matumizi ya mitandao na ujuzi zaidi katika mawasiliano ya mitandao.

No comments