TAPELI MAALUFU LAKAMATWA DAR,
Na Selemani magari
JESHI la polisi kanda maalum ya jiji la Daresalaam,
limefanikiwa kumkamata Mfaume Omari Maalufu kwa jina la Mau mkazi wa magomeni
kagera kwa tuhuma za utapeli ambaye
alikuwa akitumia majina ya watu maarufu,viongozi wa serikali na viongozi wa dini vibaya ili kujinufaisha
yeyemwenyewe
Bw. Mau alikuwa akifanya utapeli huo kwa kujivisha uhusika
wawatu maarufu na kuanza kuomba fedha kwa watu mbalimbali kupitia namba za simu
ambazo amekuwa akizitoa kwa njia ya facebook,ambapo watu wengi wamekuwa
wakiamini kuwa yeye ni kweli muhusika wa cheo alichojivisha na ndipo watu hao
walipoanza kumtumia pesa kupitia namba za simu ambazo amezichapisha katika
mtandao wa facebook
| KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI KANDA MAALUM YA DARESALAAM DCP ALLY MLEGE (KUSHOTO) AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU KUKAMATWA KWA TAPELI MAARUFU HAPA JIJINI |
Akizungumza na Wandishi wa habari ofisini kwake Kaimu
Kamishina wa polisi kanda maalum ya Daresalaam Bw. Ally Mlege amesema kukamatwa
kwa tapeli huyo hatali kumekuja kufuatia taarifa iliyotolewa na Mh.(Mb) na
mchungaji Getrude Rwakatare na kulifikia jeshi la polisi kuwa jina lake
linatumiwa vibaya na mtu anayemtakia mabaya kupitia njia ya mtandao na ndipo
uchunguzi ulipoanza na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo namba moja wa
utapeli kwa kutumia mitandao
Kamishina Mlege ameendelea kusema kuwa baada ya kukamatwa
mtuhumiwa huyo amekutwa na simu kadi mbili moja ikiwa imesajiriwa kwa jina la
Mfaume Saidi Omari yenye namba 0659736454 na nyingine ikiwa imesajiriwa kwa
jina la Alex Mtenga yenye namba 0659164744 ambazo zote alikuwa akizitumia
kuombea pesa kwa watu maalufu kwa njia ya mtandao
Kamishina Mlege ameongeza kusema kuwa mtuhumiwa huyo wa
utapeli amekiri kuhusika na utapeli wa njia ya mtandao kwa watu ambalimbali
wakiwemo wachezaji maarufu wa timu za mipira hapa nchini kwa kuvaa uhusika wa wa watu maarufu
waliostaafu, mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi na atafikisha mahakamani
ushahidi utakapokamilika
No comments
Post a Comment