Zinazobamba

Vijana kata ya mianzini wajipongeza,mwenyekiti wake awataka kuwa na moyo wa kupendana,

Na Selemani A. Magari,
Vijana wa kata ya Mianzini wilaya ya Temeke leo hii wamekutana ili kuwezakujipongeza kwa ushindi walioupata katika uchaguzi mdogo uliofanyika katika kata hiyo hivi karibuni,

Akifungua mkutano huo mwenyekiti wa vijana kata hiyo Bw. Mohamedi Mtimika amewashukuru vijana hao kwa ushirikiano waliuonyesha katika kipindi chote cha uchaguzi na kwamba kwa moyo mweupe kabisa anawashukuru sana,

Mwenyekiti wa vijana kata ya Mianzini Bw. Mohamedi Mtimika akifafanua jambo, kiongozi huyo ameahidi kutembelea mashina, makamp na matawi ili kuamsha ari ya vijana kujiunga na chama hicho
                     


 Hapa meza kuu ikiwa tayari kujibu kero za vijana, vina wengi waliojitokeza katika mkutano huo wamesema wako bega kwa bega katika kumunga mkono kiongozi wao ili waweze kujenga taasisi ya vijana imara katika kata hiyo na ikiwezekana iwe taasisi yenye nguvu ktk mkoa huu wa Daresaalam
Hapa afisa mwenezi wa vijana katika kata hiyo akifafanua jambo kwa wanachama wake

Vijana wa mianzini wakimsikiliza mwenyekiti wao

Hapa Bwana mtimika akifafanua jambo


Aidha katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amewaasa vijana wasiweke kipaumbele kuwa ni lazima wapewe Kanga, mashati na kofia ili kukipenda chama bali wajue kuwa chama ni sehemu kama hobby na sio kazi, vijana wanapaswa kufanya kazi ili wakidhi mahitaji yao

No comments