POLISI WAJIPANGA KUPAPANA NAWANAOTAKA KUVURUGA UJIO WA OBAMA, KAMISHINA ASEMA HAWATASITA KUMCHULIA HATUA YEYOTE ATAKAEHUSIKA
| Kamishina wa polisi kanda maalum ya Daresalaam akifafanua jambo kwa wandishi wa habari juu ya ujio wa wakuu wa nchi 14 wanaokuja mkutano wa smart partinaship dialogue utakaofanyika hapa nchini |
Jeshi la polisi kanda maalum ya daresalaam wamewataka wakazi wa jiji hilo kuwa waungwana kufuatia ujio wa wageni toka nchi mbalimbali kumi na nne pamoja na ule ujio wa raisi wa marekani julai mosi mapema mwezi ujao
Kamishina wa jeshi hilo kanda ya Daresalaam Suleimani Kova amesema kwa upande wao wamejipana vema kuhakikisha kuwa usalama wa wageni unaokuja unaimarisha hivyo mwananchi ama kikundi chochote atakaevunja au atakenda kinyume cha sheria hatavumiliwa na hatua kali dhidi yake zitachukuliwa
Kova amesema kwa mujibu wa taarifa za kiiterejinsia zinaonyesha kuwa kuna vyama ama vikundi fulani vinapanga kuandamana siku ya ujio wa Obama na wengine kutaka kuonyesha mabango Kwa raisi huyo, waache mpango huo maramoja kwani hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao
| Kamishina Kova akifafanua zaidi hatua zitakazochukuliwa dhidi yao |
Kova amewaomba wakazi kutoa taarifa zozote zinazohusu au zitakahusu kuharibu ujio wa Raisi Obama kwani kufanya hivyo ni kitendo cha kizalendo, Pia Kamishina huyo amewataka wahudumu wa mahoteli na uongozi kwa hotel kwa ujumla kuwa waaminifu wakati wanatoa huduma zao,kwani kufanya hivyo kutaitanganchi kwa mazuri yetu
Aidha Kamishina Kova amewataka waendesha Taxi hapa jijini kuwa wakalimu kwa wateja zao,
AIDHA katika hatua nyingine kova ametangaza kukamatwa kwa silaha kama zinavyonekana hapo chini
Kamishina kova akionyesha silaha juu kuwaonyesha wanahabari
| silaha na risasi zilizokamatwa |
KUKAMATWA KWA FEDHA ZA BANDIA HUKO MABIBO
Jeshi la polisi kanda maalum ya Daresalaam limefanikiwa kukamata pesa bandia zilizotumika kununulia mitungi ya gesi kwa Ndg. Selina Leizer huko Mabibo mtaa wa Muleba
Kamishina kova amesema watu hao walifanikiwa kununua mitungi hiyo ya gesi kwa Laiser lakini baada tu ya kuondoka katika eneo la tukio Leizer aligundua kuwa fedha zile si halali ndipo alipoendo katika kituo cha polisi magomeni kulipoti tatizo hilo, Jeshi la polisi lilimpatia askari wapelezi ili kufuatilia kesi hiyo;
Baada ya msako mkali walifanikiwa kuwakamata watumiwa watano ambao inasadikika ndio waliofika siku ya tukio wakiwa na gari aina ya Toyota Corina yenye namba za usajiri T366 BRT yenye rangi ya blue,Tukio hilo lilitokea june15 saa saba mchana hapo muleba
No comments
Post a Comment