MTOTO WA MWANDISHI WA HABARI MOSHI SAIDI AHITIMU DARASA LA 7.
Na Mwandishi wetu.
Mtoto wa Mwandishi wa habari mkongwe nchini Moshi saidi, Sasha Moshi alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wahitimu 342 wa darasa la Saba katika shule ya msingi mtambani iliyopo Boko Bunju manispaa ya kinondoni jijini Dar es salaam waliofanya sherehe za mahafali Agosti 22, 2026.
Akizungumza na waandishi wa habari katika sherehe za mahafali hayo yaliyofanyika shuleni hapo, Moshi amesema anajivunia kwa binti yake huyo kuelekea kuhitimu masomo yake ya darasa la saba mwaka huu na kusema kila mzazi ndoto yake ni kuona mafanikio ya mtoto katika taaluma na kusonga mbele zaidi katika safari yake hiyo ya kimasomo kwa hatua hiyo ya awali.
Aidha Moshi amesema hatua ya mtoto wa kike kumaliza katika hatua hiyo ni jambo jema na inaleta picha halisi ya ukimwaandaa vyema mtoto wa kike katika mwendelezo wa elimu ni zao litakalokuja kuleta matunda kwa manufaa ya baadae ya kuwa na viongozi wanawake wajasiri watakaoleta chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kuwa viongozi watakaokuwa na mchango kwa Taifa lao.
"Kwakweli nimefurahi mno hii leo kwa binti yangu kuhitimu masomo yake ya darasa la saba haikuwa safari nyepesi, ni ndoto ya kila mzazi kuona mtoto wake anamaliza masomo yake kwa mafanikio zaidi, na siku zote tukiwawezesha wanawake wanaweza" alisema Moshi.
Moshi amewashauri wazazi kusimama imara juu ya malezi ya mtoto wa kike kwa kuwapeleka shule kwakuwa ni watoto ambao wanahitaji kuendelezwa ili kuja kuwa viongozi watakaokuwa na maono na mchango mkubwa wa kukuza uchumi wa nchi katika nafasi mbalimbali,
watakazoaminiwa huku akisifu juhudi za Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia suluhu Hassan kwa namna anavyowajali na kuwathamini watoto wa kike kwa kuwaamini na kuwateua katika nafasi mbalimbali za kiutendaji serikalini.
Katika mahafali hayo yaliyofana ilishuhudiwa takribani wanafunzi 342 wakihitimu masomo yao na kuelekea katika hitimisho la mtihani wa Taifa wa darasa la saba utakaofanyika mwezi ujao nchini kote.

No comments
Post a Comment