DUA YAKUMUOMBEA RAIS DKT.SAMIA YAFANYIKA KATIKA MSIKITI WA MASJID TAQWA.
*Shekhe Mwaipopo ampongeza Rais Dkt.Samia kwa Maendeleo.
Na Mwandishi Wetu.
Dua maalumu ya kumuombea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imefanyika leo Agost 23,2026 katika Msikiti wa Masjid Taqwa uliopo Bungoni,Dar es Salaam ikiongozwa na Shekhe Mwaipopo.
Akizungumza wakati wa Dua hiyo Mwaipopo amempongeza Rasi Dtk.Samia kwa jitihada kubwa anazozifanya kwa ajili ya kuliletea Taifa maendeleo huku akiwashangaa Viongozi wa Vyama vya siasa wanaobeza jitihada hizo.
"Napenda kutumia fursa hii kumpongeza Rais Dkt.Samia kwa hatua mbalimbali za maendeleo anazozifanya ikiwemo kuzindua mradi wa umeme Bwawa la Nyerere huko Rufiji Mkoani Pwani (JNHPP)"amesema Sheikh Mwaipopo
Halikadhalika Sheikh Mwaipopo amewasihi viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuiga mfano wa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho,Freeman Mbowe kwa kushiriki katika shughuli za kitaifa,ikiwemo uzinduzi wa mradi wa JNHPP uliyofanya Agost 22,2026.

Vilevile Shekhe Mwaipopo amemshauri Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche kufanya siasa zinazoleta umoja wa kitaifa na kuweka mshikamano katika shughuli za maendeleo ya Taifa.
"Ifike hatua Heche abadili hizi siasa za kuleta mgawanyiko katika Taifa,afanye siasa zinazoleta mshikamano na umoja ili Taifa letu liweze kusonga mbele kimaendeleo na kuondoa chuki"amesema Sheikh Mwaipopo.





No comments
Post a Comment