Zinazobamba

JKT NA JWTZ ZAPONGEZWA KWA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA

Na Mussa Augustine 

Viongozi wa  Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)wampepongezwa kwa juhudi wanazozifanya za kuimarisha ulinzi na usalama nchini.

Pongezi hizo zimetolewa Julai 6,2026 na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maneosho ya 50 ya biashara ya kimataifa jijini Dar es Salaam  Sabasaba

Aidha amesisitiza kuwa vyombo hivyo vya ulinzi vimekuwa vikiendelea kulinda amani ya nchi, jambo linalowezesha wananchi kufanya shughuli za maendeleo na kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya 2050.

Amesema shirika  la JKT linafanya kazi za uzalishaji mali pamoja na kuwafundisha vijana, hatua inayosaidia kuwaandaa kujitegemea na kujiajiri.

Ameeleza kuwa kupitia maonesho hayo, taasisi hizo zimepata nafasi ya kuonesha shughuli mbalimbali zinazofanyika kwenye vikosi vyao, ikiwemo kutoa huduma kwa wananchi na mafunzo kwa vijana.

Amesema kampuni ya usafi na unyunyuzi dawa ya SUMAJKT ambayo imefanikiwa kuajiri vijana 4,800, hatua inayoonesha mchango wa taasisi hizo katika kupunguza changamoto ya ajira nchini.

No comments