KAMANDA MULIRO AWAPONGEZA ASKARI 32 WALIOFANYA VIZURI ZAIDI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Muliro Jumanne Muliro amewapongeza Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali 32 waliofanya vizuri zaidi katika utendaji kazi za Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Pongezi hizo zimetolewa leo Juni 02, 2026 katika viwanja vya bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay Kinondoni ambapo Kamanda Muliro alimwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camillus Wambura ikiwa ni sehemu kutambua mchango wa askari hao katika kazi za Polisi
Aidha, Kamanda Muliro amewataka Maofisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kusimamia sheria za nchi kwa kuzingatia sheria, nidhamu, weledi na ujasiri.
No comments
Post a Comment