Zinazobamba

CHUO CHA UREMBO CHA LISSA COLLEGE CHAZINDUA NYWELE MPYA.

Na Mussa Augustine 

Chuo cha urembo cha Lissa College kimezindua bidhaa yake mpya ya nywele inayojulikana kama (Lissa luxury hair) ikiwa lengo ni kuwajali wateja wanaopata huduma kwenye chuo hicho.

Hayo yamesemwa leo Juni 5,2026 na Mkurugenzi na mmiliki wa chuo hicho,Lissa Leonce wakati akizungumza na waandishi wa habari nakubainisha kuwa wamekuja na bidhaa hiyo baada ya kufanya utafiti wa kina wa soko la bidhaa za nywele hapa nchini na kuamini kuwa bidhaa yao itashika soko la urembo.

Amesema kuwa maono ya chuo hicho ni kwamba, watazidi kubuni bidhaa za nywele ambazo zitaendana na uhalisia wa waafrika na zenye Muonekano wa asili ambapo pia zitakuwa na bei ambazo Kila mtanzania ataweza kuzimudu.Aidha ameongeza kuwa kupitia bidhaa hiyo mpya ambayo itapatikana maduka yote kote nchini na vyuo vyote vya Lissa itakuwa mkombozi kwa wafanyabiashara ambapo pia watatangaziwa biashara zao bure kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Hata hivyo katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo amesema watatoa mkono wa shukrani kwa mama wachungaji hamsini (50) kwa kuwafuata popote walipo na kuwasuka nywele sambamba na kuwatengeneza kucha bila malipo.Hata hivyo chuo hicho pia kimemtambulisha Pinela Justine pamoja na mwanahabari Maimatha Jesse kama mabalozi wa bidhaa hiyo mpya ya nywele ambao watazunguka kufanya kampeni ya kutangaza bidhaa hiyo kote nchini.                     Maimatha Jesse                      Pinela Justine 


No comments