TLP YAMUOMBA JAJI MUTUNGI KUTOA MAFUNZO YA MARA KWA MARA KUHUSU SHERIA YA GHARAMA ZA UCHAGUZI.
Mwenyekiti TLP Taifa Richard Lymo
Na Mussa Augustine.
Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Party(TLP)Richard Lymo amesema kwamba kuanzishwa kwa sheria ya gharama za uchaguzi ambayo umeanza kutumika tangu uchaguzi Mkuu wa 2020 imesaidia kuvifanya Vyama kuwa na matumizi mazuri ya fedha na kuepuka ubadhilifu.
Lymo amesema hayo jijini Dar es salaam wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari ofini kwake Magomeni jijini humo,nakubainisha kuwa ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa imefanya vizuri kuanzisha sheria ya gharama za uchaguzi nakwamba kinachotakiwa kwa sasa ni kutoa elimu ya kutosha kwa Viongozi wa Vyama hivyo .
Aidha amesema kwamba baadhi ya Viongozi wa Vyama vya siasa wakiwemo makatibu wakuu,wakurugenzi wa uchaguzi wa Vyama wamekua na changamoto ya kushindwa kujaza taarifa muhimu zinazotakiwa kuwasilishwa kwa ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa.
Msajili wa Vyama vya siasa Jaji Mstaafu France's Mutungi.
"Hivi karibuni ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa iliitisha mafunzo ambayo yalihusu sheria ya gharama za uchaguzi,haya mafunzo ni muhimu sana yatolewe mara kwa mara kwa aviogozi wa Vyama vya siasa ili kusaidia kurahisisha uelewa mpana wa kujaza na kuwasilisha taarifa za wagombea kabla na baada ya uchaguzi"amesema Lymo.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amesema kuwa chama cha TLP hivi karibuni kinatarajia kuanza maandalizi ya kukijenga chama kuanzia ngazi za shina ili kuongeza Wanachama kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2030,ili kuwezesha chama hicho kushika hatamu katika uchaguzi huo.
"Tunahitaji kuanza maandalizi ikiwemo kuandaa mfumo wa kusajili wanachama wapya nakuwapatia kadi,ili kuweza kuimarisha chama chetu,uchaguzi wa 2030 haupo mbali hivyo inahitajika kuanza mapema maandalizi ya kuimarisha cham ili kupata wagombea wenye sifa na uwezo mkubwa wa kufanya ushindani kwenye siasa."amesema.


No comments
Post a Comment