PROF.LIPUMBA AKABIDHI RASMI OFISI,AWAAGA WANACHAMA WA CUF.
*Adai ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa imehusika kumn'goa katika uchaguzi uliyofanyika februari 21 mwaka huu.*Aonesha kutoridhishwa na kuchaguliwa kwa Hamad Masoud kuwa katibu Mkuu wa chama hicho.
*Asema yupo tayari kushirikiana na uongozi mpya na Wanachama kujenga CUF.
Na Mwandishi Wetu.
Amesema hayo leo Machi 29,2026 Makao makuu ya CUF yaliyopo Buguruni jijini Dar es salaam wakati akikabidhi rasmi ofisi na msimamo wa chama kwa uongozi mpya unao ongozwa na Mwenyekit Taifa Mirambo Camil Yusuph.
Hata hivyo amebainisha kuwa uchaguzi wa CUF uliyofanyika February 21,2026 kwa lengo la kupata Viongozi wapya wa chama hicho kutokana na barua ya Msajili wa Vyama vya siasa kuelekeza kurudiwa kwa uchaguzi kwa madai kuwa uchaguzi uliyofanyika Desemba 2024 haukufuata taratibu na kanuni za uchaguzi kuwapata Viongozi wa ngazi za juu zilikua ni njama chafu zilizofanywa na msajili wa Vyama vya siasa.
Aidha amesema kuwa pamoja na kuondoelewa kwake katika nafasi hiyo ameuomba uongozi mpya ukiongozwa na mwenyekiti mpya Mirambo Yusuph na wenzake kuhakikisha wanaimarisha chama,pamoja nakuendelea kudai katiba mpya itokanayo na maoni ya Wananchi.
"Wito wangu kwa wanachama wote tuendelee kujenga chama chetu,tuendelee kudai katiba mpya itokanayo na maoni ya wananchi,hali ya nchi yetu ni mbaya sana,vijana wengi hawana ajira,wamekata tamaa,tunapaswa kurejesha tabasamu kwa Wananchi"amesema Profesa Lipumba
"Nakuwaasa kuwa"Hamuwezi kuwa na katibu Mkuu(Hamad Masoud)ambaye alishindwa kurejesha fomu ya ugombea uraisi Zanzibar hadi tukakosa mgombea,halafu huyu ndo mnampitisha kuwa katibu Mkuu wa chama, hapo tunajidanganya,hilo naomba niweke wazi,tunaelekea kukifuta hiki chama hivyo tunapaswa kuwa makini."
Naye Mwenyekiti mpya wa chama hicho Bw.Milambo Camil Yusuamemshukuru Profesa Lipumba kwa kujitokeza kuaga Wanachama,kwani ametumikia Chama hicho kwa zaidi ya miaka 26,hivyo amekua mwalimu mzuri wa siasa.
"Sisi tumepokea msimamo wa chama,yale ya kitaasisi nitayapitisha kwenye vikao ili tuyajadili,kama mnakumbuka mara nyingine uchaguzi uliopita tulisema hatushiriki lakini tulikwenda kwenye meza ya maridhiano hadi tukarudi kwenye uchaguzi"amesema
Nakuongeza kuwa msimamo huu utaenda kulingana na makubaliano kwenye vikao vya chama,na ninaamini haya yote yalioshauriwa tutayafanyia kazi,Prof Lipumba kama mzee wetu tunaendelea kumuekea mazingira ya kutupatia maoni,mawazo na ushauri ili chama chetu kifikie malengo yake".
Aidha amehitimisha kwa kuwaomba Wanachama kuendelea kuwa pamoja,nakwamba migogoro ya kiuongozi ndani ya chama haijaanza hivi karibuni bali wamekua wakiingia kwenye migogoro lakini wanaimaliza,hivyo kwasasa washikamane ili waweze kufikia malengo yao ikiwemo kushika dola.
No comments
Post a Comment