Zinazobamba

KAMPUNI YA FORTUNE PAPER GROUP YA KICHINA YAWEKEZA SHILINGI BILIONI 154 NCHINI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya Fortune Paper Group kinachomilikiwa na raia wa China,ambayo imewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 154 nchini Tanzania tangu mwaka 2022,inaomba msaada wa sera kutoka serikalini ili kulinda biashara yake ya uzalishaji inayotegemea urejelezaji dhidi ya kile inachokiita ushindani usio wa haki kutoka kwa bidhaa za bei nafuu zinazoagizwa kutoka nje.

Katika mahojiano maalum yaliyofanyika pembeni ya maonesho ya Siku ya Kimataifa ya Zero Waste yaliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja,kampuni hiyo imesema inapanga kupanua uzalishaji na kuimarisha uwekezaji wake wa muda mrefu nchini Tanzania,ambao kwa sasa inaajiri zaidi ya wafanyakazi 150 wazawa.

Maonesho hayo yamefanyika leo Machi 30,2026 jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Kimataifa ya Zero Waste nakuhudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira Mh.Hamad Yusuf Masauni.

Akizungumza Meneja wa Biashara wa Kiwanda cha Fortune Paper,Colin Yang, alisema kampuni hiyo hukusanya karatasi taka kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania na kuzigeuza kuwa bidhaa za kufungashia zinazotumika kwa masanduku, bahasha na matumizi mengine ya viwandani.

“Hii ndiyo malighafi yetu,tunakusanya karatasi taka kote nchini na kuzibadilisha kuwa bidhaa kwa ajili ya aina mbalimbali za ufungashaji,” amesema Yang

Akielezea uwekezaji huo kuwa ni biashara pamoja na mchango katika ajenda ya uendelevu wa mazingira nchini Tanzania.

Kampuni hiyo imeanza shughuli zake nchini Tanzania mwaka 2022 na tangu wakati huo imewekeza zaidi ya dola milioni 60 katika uwezo wa uzalishaji wa kiwanda na shughuli za ndani, kwa mujibu wa Yang.

Aidha ameongez kuwa kiwanda cha Fortune Paper kina nia ya kupanua bidhaa zake pamoja na kuongeza uwekezaji wa mtaji kutokana na matarajio ya ukuaji wa muda mrefu wa mahitaji ya ndani ya nchi.

Hata hivyo,Yang amesema biashara hiyo inakabiliwa na shinikizo kutoka kwa bidhaa za karatasi zinazoagizwa kutoka nje, hasa kutoka India na China, ambazo alisema zinaingia katika soko la Tanzania chini ya utaratibu wa msamaha wa ushuru unaoziruhusu kuepuka kodi zinazolipwa na wazalishaji wa ndani.

No comments