Zinazobamba

MGOMBEA MWENZA ADA -TADEA AVULIWA UANACHAMA.

Na mwandishi wetu

Kamati kuu ya Chama Cha ADA -TADEA iliyokutana leo jijini Dar es salaam imewavua uanachama wanachama wake kadhaa ikiwemo Mgombea mwenza wa urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu,kutokana na kukiuka taratibu mbalimbali za chama hicho.

Waliovuliwa uanachama ni pamoja na aliyekuwa mgombea mwenza chama hicho, Ali Makame Issa,Katibu wa  Baraza la Vijana, Alphonce Mayunga na Katibu  Mkoa wa Mwanza, Deusdedit Tiba.

Akizungumza wakati akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari mapema leo Novemba 19,2025  jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa ADA_TADEA, Salehe Msumari amesema kuwa kamati hiyo imefikia uamuzi huo kutokana na wanachama hao kukiuka taratibu za chama,nakwamba tayari nafasi za viongozi hao zimeshajazwa na taarifa hiyo itapelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa.

Amesema wagombea hao wamevuliwa uanachama kwa sababu mbalimbali na kwamba kuanzia sasa matamko ambayo yamekuwa yakitolewa na aliyekuwa mgombea mwenza hayatatambuliwa na chama hicho.

Msumari mesema nafasi ya Makamu Mwenyekiti  Zanzibar imechukuliwa na Ally Mohamed  kutokana na aliyekuwepo  kuhamia chama kingine cha siasa.

Amesema pia wamejaza nafasi nyingine Makamu Mwenyekiti Bara, ambaye ameumwa muda mrefu sana na nafasi hiyo kukaimishwa kwa Farida Abdallahna Katibu Mkuu Mwenezi ambaye alihama chama hicho na nafasi yake kuchukuliwa na Mwenyekiti mkoa wa Simiyu, Luhende Kassim,  na nafasi ya Katibu wa Vijana kuchukuliwana Suzan Thomas.

Kuhusu uchaguzi amesema chama hicho hakijapata nafasi yoyote ya uongozi na kwamba Kamati hiyo imekutana kujadili kuona walipokosea na kuwa na mapendekezo ndani ya chama ya nini kitakachofuatwa.Katika hatua nyingine chama hicho kimempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa hotuba yake aliyoitoa hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ameomba kuwepo kwa maridhiano ili kuweza kulinusuru Taifa kutokana vurugu ambazo zilitokea wakati wa uchaguzi nakusabisha vifo,wizi na uharibifu mkubwa wa mali za watu.

Aidha Mwenyekiti wa Chama hicho,Juma Ali Khatib amesema wanampongeza Dkt Samia kwa hotuba nzuri hususani alipotoa msamaha kwa walioshiriki katika vurugu za Oktoba 29, siku ya uchaguzi. 

"Sisi kama ADA-TADEA tunampongeza sana rais Dkt Samia kwa kutoa msamaha kwa Vijana waliofuata mkumbo wa maandamano,pia tunawasihi Vijana waache kujiingiza kwenye maandamano kwa kufuata mkumbo,tunaomba wawe watulivu,wastahimilivu,wasubiri kamati iliyoundwa kushughulikia maridhiano"amesema Khatib. 

No comments