DC MSANDO MGENI RASMI TAMASHA LA MWANAMKE AFYA FUN RUN & SPORTS BONANZA.
*Wananchi waombwa kujitokeza kwa wingi.
Na Mwandishi Wetu.
Hayo yemesemwa leo Novemba 19,2025 Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa taasisi hiyo Asmin Kihemba nakubainisha kuwa hatua hiyo ni kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwezesha watanzania kupata bima za Afya.
"Utaratibu Wetu wa kutoa bima za Afya tumezingatia makundi yote,tuna wagusa wajane,watu wenye uhitaji maalumu,Wanawake wasiojiweza ikiwa ni kuleta chachu ya kuwaonesha kwamba bima za fya zina umuhimu,nakatika miaka yetu hii mitatu ya Mwanamke Afya Fun Run tunashukuru Mungu tumeweza kugusa wanawake zaidi ya mia saba(700) na tukienda kutoa bima za Afya kipindi hiki cha msimu wa tatu tutakua tumefikia watu elfu moja(1000)ambao wameguswa na hizo bima"amesema Bi.Kihemba.
Kwa upande wake Afisa habari wa Mwanamke Afya Fun Run Pamela Mwakasagule amesema kwamba taasisi hiyo imekua ikifanya bonanza hilo kila mwaka ambapo mwaka huu ni msimu wa tatu likiwa na lengo kuu kwa ajili ya kutoa bima za Afya kusaidia wahitaji wa makundi maalumu ambao ni wajane,watu wenye uhitaji,pamoja na wazee.
"Mwaka jana tuliweza kutoa bima 450,lakini mwaka huu tunatarajia kutoa bima 700 na lengo kuu la Mwanamke Afya Fun Run kufanya mabonanza haya na kutoa bima hizi ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita ili kila Mtanzania aweze kua na bima ya Afya,hivyo tunafanya michezo lakini wakati huohuo tunajali afya za Wananchi wa Tanzania" amesema Bi.Mwakasagule.
" Nakuongeza kuwa"utaratibu ni kwamba kwa wale wasiojiweza tayari tumeshaanza kuorodhesha majina yao kwa ajili ya kuwapatia hizo bima,lakini wengine watapata bima pale watakapofika Viwanja vya barafu,lakini kwenye michezo hii kuna zawadi moja ya zawadi itakayokuwepo ni kupata bima ya Afya".
Nae Afisa habari namba mbili wa taasisi hiyo MC Ande Makopa amebainisha kuwa bonanza hilo litakua na michezo mbalimbali ikiwemo,kuvuta kamba,kukimbiza kuku,kukuna Nazi,kukimbia na yai,kukimbia na Maji kichwani,kukimbia na magunia pamoja na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.
Vilevile Mratibu wa bonanza hilo Joseph Katembo amesema kwamba bonanza hilo halina kiingilio,huku akibainisha kuwa Taasisi hiyo haipokei watu wenye uhitaji bila kupata uthibitisho kutoka mamlaka za uongozi anakoishi muhitaji huyo kama vile viongozi wa Serikali za Mitaa.
"Taarifa za uthibitisho na uhalali wa kupata watu wenye uhitaji unatoka kwenye mamlaka za uongozi kutoka ngazi za Wilaya hadi Mitaa"amesema Katembo.
Hata hivyo Rosemary Madafu(MC Madafu)amesema kuwa tamasha hilo limedhaminiwa na WCF, Maji ya uhuru,vyombo vya ulinzi na usalama(Suma JKT).






No comments
Post a Comment