Zinazobamba

BUSANDA YA KUMBUKWA KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI LA DKT.SSH.


Na Mwandishi wetu 

Wananchi wa  Jimbo la Busanda, wamepongeza DKT.Jafari Seif kwa kuteuliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  DKT .Samia Suluhu Hassan  Mbunge wao kuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI anayeshughulikia Afya.

Wakizungumza  kwa nyakati tofauti wamesema ni heshima ya kipekee ambayo haijawahi kutokea tangu jimbo hilo kuanzishwa Ambapo uteuzi huo umeleta faraja na matumaini mapya kwao huku wakieleza kuwa kwa mara ya kwanza Busanda imepata mwakilishi wa ngazi ya Uwaziri serikalini.Wameeleza kuwa uteuzi huo unathibitisha dhamira ya Rais  DKT.Samia Suluhu Hassan,kuhakikisha maeneo yote yanashirikishwa kikamilifu katika maendeleo ya Taifa hususani kundi la vijana.Sambamba na hilo Wakatoa ombi kwa mbuge wao awajengee    barabara ya Geita - Kahama kwa kiwango cha lami  kwani kwa kufanya hivyo itafungua fursa za kiuchumi na kupunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa wilaya hiyo na maeneo jirani.Pia  wakatoa kilio chao kwa Serikali Kwenye Sekta ya afya   kupitia Dkt. Jafari ili  kuboresha vituo vya afya na zahanati kwa kuongeza dawa, vifaa tiba na huduma za uhakika muda wote ili kupunguza usumbufu kwa wananchi wanaohitaji matibabu.


No comments