Zinazobamba

REA YAENDELEA NA UUZAJI WA MAJIKO YA GES KWA BEI YA RUZUKU

Na Mwandishi wetu 

Wakala wa Nishati Vijijini ( REA) wamekuja na Majiko mia Tano kwenye maazimisho  ya siku ya chakula Duniani yanayofanyika Katika viwanja vya usagara Jijini Tanga yenye kauli mbiu inayosema, Tuungane pamoja kupata chakula Bora kwa Maisha Bora ya Badae,yaliyozinduliwa jana Oktba 11,2025, na mku wa mkoa wa Tanga Mhe, DKT. Batida Buriani.

Afisa Mawasiliano kutoka REA ndugu Steven Nyamiti amebainisha kuwa kwenye maazimisho hayo yanayoendele Hadi Oktba ,16,2025, wamekuja na majiko mia Tano ya Ges ambayo yanauzwa kwa bei ya ruzuku hivyo Wananchi wa mkoa wa Tanga waje kwa wingi kwenye viwanja vya Usagara ili wajipatie majiko.Amesema Wananchi wanatakiwa  kuja na vitambulisho vya Taifa (NIDA)  wakifika kwenye Banda Hilo watasajiliwa Kisha watalipa kiasi Cha T, sh elifu kumi na Saba na Mia Tano tu

Naye Akida veso Mkazi wa Donge,Jijini Tanga ameishukuru Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuja na kampeni ya uuzaji wa majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku.

Ameogeza kuwa wafike na Vijijini uko ili Wananchi waishio uko nao wapate Nishati hiyo waepuke kutumia Nishati chafu na uharibifu wa Mazingira Naye Bi Mwamvua Mkazi wa Chumbageni Mkoani tanga amefurahishwa na REA kwa kuwaletea majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku,na ametumia Fursa hiyo kuwaasa wanawake wenzake kumuunga mkono Mhe DKT. Samiha Suluhu Hasan Rais, wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuwa kina wa Nishati safi

No comments