ZIARA YA DKT. NCHIMBI YALETA NEEMA JIMBO LA BUKENE
Na. Zuhura Rashid - Nzega
Mgombea mwenza nafasi ya Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt Emmanuel Nchimbi leo octoba 4, amefanya ziara katika Jimbo la Bukene wilaya ya Nzega, kwa lengo la kunadi sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea uchaguzi mkuu utakao fanyika mwaka huu oktoba 29
Dkt Nchimbi amewaahidi wananchi wa Jimbo la Bukene kuwa katika miaka mitano 5 ijayo iwapo Chama Cha Mapinduzi apinduzi (CCM) kikipata ridhaa ya kuongoza kitajenga soko la kisasa katika Jimbo hilo, kwa ajili ya kuuza uchumi wa halmashauri ya wilaya ya Nzega
Kwa upande mwengine Dkt Nchimbi amesema wamedhamiria kuboresha mazingira ya biashara ili kufanya mamlaka ya kodi kujenga urafiki na kuwapa elimu wafanya biashara, kwani kwa kufanya hivyo kutawafanya wananchi kulipa kodi bila ya kushurtishwa
Naye Mgombea wa Ubunge Jimbo la Bukene, John Stephano Luhende amesema mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) umepita katika Jimbo hilo, mradi huo utawasaidia wananchi wa Bukene na Nzega kwa ujumla kuweza kusafiri kwa haraka pamoja na kupata fursa mbalimbali wakati wa ujenzi na baada ya kumalizika kwa mradi huo.
Luhende amesema katika uongozi wake atapanua wigo wa usafirishaji wa mawasiliano katika Jimbo la bukene, kwa kujenga barabara zote zenye changamoto, barabara hizo ni kutoka Bukene mpaka Mambali, kutoka Mambali mpaka Lubisu, kutoka Tabora Mambali, Semembela mpaka Kahama mjini.
Amesema barabara hizo zitaenda kugusa maisha ya watu na kuwa na manufaa makubwa kwa maendeleo ja Jimbo la bukene
No comments
Post a Comment