SALUM OMARY KUSHUGHULIKIA KERO YA BARABARA,AFYA NA USALAMA KATA YA PUGU STESHENI.
Mgombea udiwani kata ya Pugu Stesheni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Salum Shaibu Omary amesema kuwa endapo Wananchi watamchagua kuwa diwani wao atahakikisha anashughulikia kero mbalimbali ikiwemo Miundombinu ya barabara.
Omary amesema hayo mwishoni mwa wiki katika Kata ya Pugu Stesheni Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari nakubainisha kuwa Kata yake ina changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa miundombinu ya Barabara,huduma za Afya pamoja na kukithiri kwa vitendo vya uhalifu.
"Miundombinu ya barabara katika kata yangu ni hafifu na hairidhishi kwa kiwango fulani,Mungu akinijalia nikiwa diwani wa kata hii nitaenda kusimamia hilo kwa na Mgombea ubunge Ukonga Jery Slaa,kutengeneza barabara hii inayotoka pugu stesheni-mnadani, na mnadani-Gongolamboto na ile ya mnadani kupitia Kisukuru,ambapo kuna mapori ambayo yanatishia usalama wa Wananchi" amesema Omary
Nakuongeza kuwa"nitaenda kuwapambania Wananchi kuhusu barabara itokayo mnadani kupitia kivuko cha mto Msimbazi kuingia mtaa wa bangulo,pale kwenye Mto wa Msimbazi kuna changamoto ya daraja,zikinyesha mvua kubwa tunapata maafa kwa Watoto wetu,kushindwa kuvuka,au kudumbukia kwenye Mto nakupoteza maisha "
Akizungumzia kuhusu changamoto katika Sekta ya Afya, Mgombea huyo wa udiwani amesema kuwa kata hiyo inahitaji Zahanati nzuri ya kisasa,yenye kutoa huduma zote kwa Wananchi nakwamba Zahanati iliyopo kwa sasa ina upungufu wa baadhi ya huduma muhimu.
"Wananchi wakishanipa ridhaa ya kuwa diwani wa kata hii nitaenda kupambana kadri ya uwezo wangu kuhakikisha huduma zote katika Zahanati ile zinapatikana,pia nitapambana kupata kituo kingine cha afya kwasabubu Zahanati iliyopo iko mbali kutoka mtaa wa Kichangani kwenda mtaa wa Bangulo,hivyo Wananchi wanapata usumbufu wa kupata huduma inapotokea dhalura" amesema Omary.
*Hali ya usalama kwa Wananchi.
Mgombea huyo wa udiwani Kata ya Pugu Stesheni amesema kuwa kwa sasa hali ya usalama katani humo haipo sawa,hivyo anahitaji kupambana ili kijengwe kituo cha polisi cha kata,pamoja na kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi kwa ajili ya kulinda raia na mali zao,na kutokomeza vitendo vya uhalifu.
*Kuinua Vikundi vya akina mama na Vijana wajasiriamali.
Aidha Omary amesema kuwa ana mpango wa kuinua Vikundi vya akina mama na vijana wajasiliamali wa kata ya Pugu Stesheni kwa kuwezesha kupata Mikopo ya kuendeleza biashara zao kutoka kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
"Kuna baadhi ya makundi yanalalamika kwamba yameomba mikopo muda mrefu,miaka miwili hadi mitatu iliyopita bila mafanikio,ukiangalia wana vigezo vya kukopeshwa sasa sijajua changamoto hizi zinatokana na nini,nitakapokuwa diwani nitaenda kufuatilia hili suala kwa ukaribu zaidi ili wakina mama na vijana wapate mikopo hiyo."amesema Omary.
Nakuongeza kuwa,Mimi(Salum Omary)nitaenda kupambana na vijana wenzangu kutokomeza umasikini na kuwapa Elimu ya kujiajiri ilimradi wapate fursa ya kutengeneza maendeleo katika kata yetu kupitia Vijana."
*Amuombea kura za ndio Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga Jerry Slaa.
Aidha Omary ametumia fursa hiyo kuwaomba Wananchi wa kata ya Pugu Stesheni na maeneo mengine kumpigia kura za ndio za kutosha Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na mgombea ubunge jimbo la Ukonga Jerry Slaa ili aweze kufanya nae kazi kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Pugu Stesheni.
No comments
Post a Comment