MADILU AAHIDI KUSHUGHULIKIA BEI YA MAZAO YA UFUTA,MBAAZI NA KOROSHO LULINDI.
Musa Said Dadi "Madilu"
Mgombea ubunge jimbo la Lulindi Wilayani Masasi Mkoani Mtwara kupitia Chama Cha Wakulima (AAFP)Mussa Saidi Dadi "Madilu"amewaomba Wananchi wa jmbo hilo kumpigia kura za ndio kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 29 mwaka huu ili aweze kutatua kero mbalimbali za kijamii na kiuchumi zinazowakabila Wananchi hao.
Na Mwandishi Wetu:Masasi Mtwara.
Akizungumzia Septemba 26,2025 katika kata ya Chiungutwa jimbo la Lulindi wakati akinadi Ilani ya chama hicho na kuwaomba Wananchi kumchagua awe Mbunge wao,amesema kuwa Wananchi wa jimbo hilo wanakumbwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa soko la uhakika la mazao wanayozalisha hivyo akipewa ridhaa atahakikisha anawatetea wakulima wauze mazao yao kwa bei nzuri.
Aidha amesema kuwa mfumo kuuza mazao yao kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani wakulima wamekua wakinyonywa kwa kuuza bei ya chini,huku malipo yao pia yakikaa muda mrefu hali ambayo inawafanya waishi maisha ya shida kutokana na kukosa fedha za kuendesha maisha yao.
Aidha amesema kuwa amezunguka kata zote za jimbo hilo nakujionea tatizo la wakulima ni kubwa ndio maana ameamua kugombea nafasi ya Ubunge kupitia AAFP ili kuwatetea wakulima kwani kundi hilo ndio lenye mamlaka kwenye Taifa hilo.
"Hapa katikati ya msimu nimeona namana mazao ya ufuta na mbaazi yalivyouzwa kwa bei ya chini sana, nikaona huku tunakaoenda kwenye Korosho tutaumia zaidi,nikasema lazima niwalete wakulima wenzangu waweze kuongea ili tusiendelee kuumia".amesema Dadi
Nakuongeza,tatizo lingine kwenye Kilimo ni suala la pembejeo,ambapo pembejeo zinazotolewa kwa wakulima sio za bure bali wanafanyiwa biashara kwa madai kuwa wanakatwa malipo hayo kupitia mazao yao pindi wanapouza.
Katika hatua nyingine amesema jimbo la Lulindi lina changamoto ya mawasiliano ya barabara za ndani ambapo wakulima wanapata shida kutoa mazao yao shambani nakuyapeleka sokoni,hivyo Chama Cha Wakulima (AAFP)kitaondoa adha hiyo endapo Wananchi watakipa ridhaa ya kushika dola Oktoba 29 mwaka huu.
Mark Isdori Awali Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Mark Isdori amesema kuwa kwa sasa Taifa linahitaji viongozi kuanzia ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani wanao tokana na wakulima ili kuweza kutetea haki za wakulima,hivyo amewaomba Wananchi hao kukichagua chama hicho ili kiweze kushika dola nakuleta mapinduzi makubwa ya kimaendeleo hususani kuwainua Wakulima nakuwafanya wawe na thamani.
Nae Mkurugenzi wa uchaguzi AAFP Godfrey Ten ambaye pia ni Mgombea ubunge jimbo la Kigambon Dar es salaam amesema kuwa Tanzania tangu ipate uhuru mwaka 1961 hadi sasa maendeleo yaliyopo hayafanani,hali hiyo ni kutokana na mfumo mbovu wa uongozi uliopo madarakani.
Godfrey Ten "Mfumo unatengenezwa na watu,sisi mpaka tupo hivi leo nikutokana na mfumo uliotengenezwa na Chama Cha Mapinduzi ambao tunaufuata,kwahiyo tumekuja sisi AAFP kubadilisha mfumo huu tunaomba mtupe ridhaa Oktoba 29 waka huu tuweze kushika dola tulete mabadiliko makubwa ya kiuchumi".amesema.
Rashid Maokola Vilevile Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Rashid Maokola amesema kuwa watu wa Kusini wamechoka na changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kukosa umeme wa uhakika,miundombinu mibovu ya barabara,uhaba wa maji,nakuwaomba Wananchi wakichague chama Cha AAFP kiweze kuwaondolea kero hizo.
No comments
Post a Comment