Zinazobamba

SHILINGI TRIONI 1 ZABORESHA HUDUMA ZA AFYA.

Na Mussa Augustine.

Serikali imewekeza shilingi trillioni 1 na bilioni 298 ili kuboresha huduma za afya nchini,nakuhakikisha Watanzania wanapata dawa na vifaa tiba vya kutosha.

Hayo yamesemwa leo March 1,2025 na Msemaji Mkuu wa Serikali Greyson Msigwa wakati akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam nakubainisha kuwa hatua hiyo ni kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora za afya.

Msigwa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ameeleza kuwa mageuzi makubwa yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya afya yameleta matokeo makubwa, ikiwemo kupungua kwa vifo vya wakina mama wanaojifungua kutoka 556 hadi 104 ndani ya miaka minne ya uongozi wake.

" Lengo la serikali ni kupunguza vifo hivyo hadi asilimia 70 ifikapo mwaka 2030,na lengo hili litafanikiwa kwa kiwango kikubwa kwani Rais Dkt.Samia amewekeza jitihada za mkusudi katika kuboresha huduma za afya kila kona ya nchi hii" amesema Msigwa.

Hakuna maoni