Zinazobamba

HAKUNA BIDHAA ZA VYAKULA ZILIZOPANDA BEI ZANZIBAR:CCM


Mwandishi Wetu, Zanzibar

Bei za bidhaa za vyakula Zanzibar na vitongoji vyake Zanzibar hazijapanda kama ilivyodaiwa na  Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Jussa Ismail Ladhu.

Akizungumza sokoni hapo mara baada ya ziara ya kukagua bei za bidhaa za vyakula sokoni hapo, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Muhsin Ussi ambaye aliambatana na Katibu Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema hakuna bidhaa zilizopanda.

Muhsin alisema kuwa licha ya wao kufika sokoni hapo kwa ajili ya kununua mahitaji lakini pia wamefuatilia kujua ukweli na kubaini hakuna chakula kilichopanda bei.

Muhsin alisema kuwa hivi karibuni Jussa aliviambia vyombo vya habari kuwa bidhaa katika masoko ya Zanzibar bei zimepanda kutokana na Serikali ya Mapinduzi (SMZ), kuzichelewesha meli bandarini kushusha mizigo zikiwemo bidhaa za vyakula hivyo kusababisha kadhia hiyo.

“Tumejionea bidhaa zipo za kutosha na watu wapo katika pilika pilika za manunuzi” alisema na kuongeza kuwa Rais Dk Hussein Ali

Hakuna maoni