Zinazobamba

Mbeto : Zbar kuna njaa ya upinzani kulilia madaraka

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi  (CCM) kimesema Zanzibar  hakuna njaa , wala  upungufu wa bidhaa muhimu za vyakula   au bei  za bidhaa kuwa juu kwenye Masoko   kama inavyodaiwa na upinzani.

Kadhalika chama hicho  kimetaja  shida kubwa  iliopo  Zanzibar ni upinzani kutaka kutamani madaraka kwa  kutumia mbinu batili, uzushi na uongo. 

Hayo yameelezwa na Katibu  wa Kamati Maalum  ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo  ,Khamis Mbeto Khamis, alipomaliza  kutembelea Soko  jipya la Mwanakwerekwe Mkoa  wa Mjini  Magharibi Kisiwani Unguja. 

Mbeto  alisema maisha ya wananchi lwa ujumla  yanaendelea kama kawaida,  bei za bidhaa ni  wastani , Wafanyabishara wanafanya shughuli zao ,  hakuna  aliyepandisha bei kama inavyopotoshwa kwenye mitando ya kijamii .

Alisema njaa ya   Zanzibar  ni ya kisiasa huku   wapinzani  wa CCM wakitamani  madaraka kwa kutumia  hila ,  uongo na uzushi  kwa kudai  Zanzibar kuna maisha magumu.

'Zanzibar kuna njaa ya kisiasa upinzani  unalilia madaraka kwa kutumia sera zisizoungwa mkono na  wananchi  . ACT wanalilia kushika  utawala bila kuwavutia wananchi kwa   sera makini .Badala yake wanategemea nguvu za  uzushi , unafiki na  uongo  " Alisema Mbeto 

Aidha Katibu huyo Mwenezi, alisisitiza    kuwataka viongozi  wa  ACT ,kuelewe utendajikazi uliofanywa na Serikali ya Rais  Dk  Hussein  Ali Mwinyi kqa miaka minne  ,umejenga imani kwa wananchi baada ya kutimiza ahadi  zilizoahidiwa kapitia  ilani ya uchaguzi na kuleta  maendeleo .

"Kila  kilichoahidiwa kwenye ilani na ahadi za    Rais Dk Mwinyi mwaka 2020 zimetimizwa hatua kwa hatua na kwa  wakati sahihi.  SMZ  haikutaka  kuendekeza malumbano ya kisiasa majukwaani badala yake iliweka mkazo  kusimamia  mabadililo ya kimaendeleo " Alieleza

Mbeto alisema  takribam Masoko yote   yamesheheni bidhaa  muhimu  kwa ajili ya  maisha ya kawaida  pia kuna aina zote  za vyakula kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan zikipatikana . 

Hata hivyo Mbeto aliwaasa ACT na kuwataka  waache siasa za kizushi, zinazokuza mifarakano katika kijamii   ilihali  wakijua  zama hii si  zama  ya  kutegemea udaku, uzushi na  uongo kama   mtaji wa kisiasa kwa  chama makini cha siasa

Hakuna maoni