BANDARI YA KWALA YAPUNGUZA MSONGAMANO WA MIZIGO
Na Mussa Augustine,Pwani
Serikali imewekeza Shilingi bilioni 83 katika Bandari Kavu ya Kwala ili kupunguza msongamano wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam na kuvutia wawekezaji zaidi nchini.
Bandari hiyo ina uwezo wa kuhifadhi makontena 300,000 kwa siku, sawa na mara tatu ya uwezo wa sasa wa Bandari ya Dar es Salaam.
Tayari miundombinu muhimu kama njia za treni, barabara za zege, na maghala ya kuhifadhia makontena imejengwa, hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo na kuimarisha uchumi wa taifa.
Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu waSerikai Machi 16,wakati akizungumza na Waandishi wa habari,katika kongani ya Viwanda Mkoani Pwani.
"Katika sekta ya Maji, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua mradi mkubwa wa maji Machi 9,2025 katika Wilaya ya Same, ambapo Shilingi bilioni 406 ziliwekezwa. Mradi huo utafaidisha wakazi wa Same, Mwanga, na Korogwe kwa kuwapatia huduma bora ya maji safi na salama.
Aidha, serikali imepanga kutumia Shilingi bilioni 335.9 kutekeleza mradi wa Bwawa la Kidunda, ambalo litaongeza upatikanaji wa maji katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, na Morogoro. Mbali na kuhifadhi maji, bwawa hilo litazalisha megawati 20 za umeme ambazo zitaunganishwa kwenye gridi ya taifa ili kusaidia upatikanaji wa nishati nchini.
"Miradi hii inaonesha dhamira ya serikali katika kuimarisha miundombinu na kukuza uwekezaji, hatua inayotarajiwa kuleta maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii nchini." Amesema
Post Comment
Hakuna maoni
Chapisha Maoni