Zinazobamba

WANACHUO WAFANYA TUKIO HILI,KILIBA AGUSIA UCHAGUZI MKUU 2025.


Maelfu ya wanavyuo wa Kampeni ya “Mama Asemewe” kutoka vyuo mbalimbali mkoani Dodoma wamefanya matembezi maalum kwa ajili ya kuweka maazimio kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.  

Matembezi hayo yamefanyika chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Kampeni ya Mama asemewe ya Ndg. Geofrey Kiliba, yakihusisha wanachama wa kampeni hiyo wanaounga mkono juhudi za maendeleo za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Akizungumza baada ya matembezi hayo, Ndg. Geofrey Kiliba amesema kuwa lengo ni kuonyesha mshikamano wa wanavyuo katika kuchagiza maendeleo ya taifa na kuandaa mikakati ya kuhakikisha vijana wasomi wanashiriki kikamilifu kwenye uchaguzi ujao.  

“Tunatambua mchango wa vijana katika ustawi wa nchi yetu, na kupitia Kampeni ya Mama Asemewe tunajipanga kuhakikisha tunashiriki kikamilifu katika kujenga Tanzania yenye maendeleo endelevu chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan” alisema Kiliba.  

Katika maazimio yao, wanavyuo wameeleza dhamira ya kushiriki kwa wingi katika mchakato wa uchaguzi, kuhakikisha ushiriki wa vijana unakuwa na nguvu, na kuendelea kueneza uelewa kuhusu sera na mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita.  

Matembezi hayo yamehitimishwa kwa Kongamano kubwa la Wanavyuo katika ukumbi wa Jakaya Kikwete convention centre uliowakutanisha wanavyuo, viongozi wa kampeni, na wadau mbalimbali wa maendeleo huku mgeni rasmi akiwa ni Mh Deogratius Ndejembi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambapo mipango zaidi iliwekwa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Hakuna maoni