Zinazobamba

DEREVA ALIYESABABISHA KIFO CHA KAMANDA CHIKO AKAMATWA

Na Mwandishi Wetu.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kumkamata dereva wa daladala lenye namba  za usajili T 580 EAE aina ya Tata, Elia Asule Mbugi 'Dogo Bata' (26) mkazi wa Kinyerezi kwa kosa la kusababisha kifo Cha kamanda Awadhi CHIKO.


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi jijini Dar es Salaam,SACP Jumanne Muliro,  inadaiwa dereva huyo, Machi 17, mwaka huu akiwa anaendesha daladala hiyo, alimgonga Mkuu wa  Polisi, Wilaya ya Kipolisi, Chanika, Awadhi Chico, ambaye alifariki dunia.


SACP Mulilo Jumanne Mulilo, akizungumza leo na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, amesema   baada ya dereva huyo kudaiwa kutenda kosa hilo alikimbilia Mbalizi, jijini Mbeya  ambako alitiwa nguvuni Machi,  27, mwaka huu na  kurejeshwa Dar es Salaam na muda wowote atapandishwa kizimbani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.


"Baada ya Kamanda Chiko, kugongwa na kufariki dunia, dereva anayetuhumiwa kuhusika na tukio hilo, alikimbilia Mbozi jijini Mbeya na kutokana na jitihada zilizofanywa na jeshi letu, lilifuatilia nyendo zake na kufanikiwa kumkamata na kumrejesha hapa Dar es Salaam na wakati wowote atafikishwa mahakamani baada ya taratibu za kiuchunguzi kukamilika", amesema Kamanda Mulilo.

Ajali iliyopoteza maisha ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Chanika, jijini Dar es Salaam, AS Chico, ilitokea Machi 17 eneo la Pugu Sekondari baada gari yake aina ya Prado kugongana na daladala hiyo akiwa anaelekea katika majukumu yake ya kila siku.

Kamanda SP  Chiko, alizikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam Machi 18, mwaka huu baada ya taratibu za kijeshi kukamilika.

Hakuna maoni