SERIKALI WILAYANI KISARAWE ITASHIRIKIANA NA WWF KUTUNZA MAZINGIRA: DC MAGOTI
Na Mussa Augustine,Pwani
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani Petro Magoti amesema Serikali Wilayani humo itaendelea kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira ( WWF) katika kufanikisha adhma yake ya utunzanij wa Mazingira Wilayani humo.
DC Magoti amesema hayo Machi 15 Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Ishi kijani,Ishi kijanja" iliyozinduliwa na WWF kwa ajili ya kuhamasisha Vijana na jamii kwa ujumla kutunza Mazingira.
Uzinduzi wa kampeni hiyo umeenda sambamba na maadhimisho ya Wasaa wa Mazingira( 60 biggest hour Earth) uliyofanyika katika shule ya wasichana ya Joketi Mwegelo iliyopo Wilayani humo
Amesema kwamba WWF inaishi maono ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kutunza Mazingira nakuachana na matumizi ya Nishati chafu itokanayo na kuni ambapo imekua ikichangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa Mazingira.
Aidha amesema kuwa Wilaya ya Kisarawe ina misitu mikubwa ya kuvutia na uoto wa asili ambao unahitajika kutunzwa kwa hali na mali ili kuifanya Wilaya hiyo iwe sehemu ya kuvutia watalii kutokana na kuwepo kwa vivutio vingi vya watalii kama vile eneo la KaziMzubwi.
"WWF tunawashukuru sana mmekua mstari wa mbele kuwekeza katika utunzaji wa Mazingira kwenye shule hii ya Joketi Mwegelo,niwaombe tena mshirikiane na Afisa Elimu Wetu wa Wilaya muangalie shule nyingine muwekeze ili tuzifanye shule za Kisarawe ziwe na Mazingira mazuri na watoto Wetu waweze kufaulu vizuri" amesema DC Magoti.
Nakuongeza kuwa" nawaomba WWF mje Kisarawe mfungue Ofisi yenu hapa,ili muwe karibu na maeneo yetu na hii itasaidia utekelezaji mzuri wa majukumu yenu katika uhifadhi wa Mazingira katika Wilaya ya Kisarawe " amesisitiza.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa WWF Nchini Tanzania Yohana Mpagama amesema kwamba shirika hilo limetoa majiko mawili ya kupikia ambayo hayatumii kuni kwa asilimia 60,hivyo yanasaidia kuondokana na matumizi ya Nishati chafu ambayo inasababisha uharibifu wa Mazingira.
Amesema kwamba WWF imekua ikifanya shughuli zake kwa muda wa miaka 30 sasa katika uhifadhi wa Mazingira nakwamba litaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kudhibiti mabadiliko ya Tabianchi.
SERIKALI WILAYANI KISARAWE ITASHIRIKIANA NA WWF KUTUNZA MAZINGIRA: DC MAGOTI
Reviewed by mashala
on
16:55:00
Rating: 5

Post Comment
Hakuna maoni
Chapisha Maoni