Zinazobamba

RAIS MWINYI:TUSIPANDISHE BEI ZA BIDHAA ZA VYAKULA WAKATI WA RAMADHANI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuridhishwa  na upatikanaji wa Bidhaa za Vyakula na kuwataka Wafanyabiashara Kutopandisha Bei  wakati Ramadhani itakapoanza.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipotembelea Masoko ya Jumbi , Mwanakwerekwe na Darajani  kuangalia Mwenendo wa Biashara  na Upatikanaji wa Bidhaa za Vyakula  kuelekea Mwezi Wa Ramadhani.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi  ameeleza kuwa Serikali inajipanga kwa ajili ya Ujenzi wa Masoko mengine maeneo mbalimbali ili kila Mfanyabiashara afanye biashara  kwenye mazingira  rasmi .Kuhusu Suala la  Usafi wa Masoko ameuagiza Uongozi wa Masoko hayo kutafuta njia Bora zaidi ya Uhifadhi wa Bidhaa za Wafanyabiashara ili Masoko kuwa safi wakati Wote.Amezielekeza Taasisi zinazosimamia Masoko hayo kuhakikisha Upatikanaji wa  Huduma ya Maji  na Vipooza hewa katika Masoko yote pamoja  na kuimarisha Usafi.

Ziara hiyo ya Rais Dkt, Mwinyi ni ya Kwanza tangu kufunguliwa kwa Masoko Mapya ya Jumbi , Mwanakwerekwe na Ukarabati Mkubwa wa Soko la Darajani.



Hakuna maoni