Zinazobamba

DIWANI SAADY KHIMJI KUMCHANGIA FOMU YA UBUNGE ,MBUNGE ZUNGU


NA HERI SHAABAN (ILALA )

DIWANI wa kata ya Ilala SAADY KHIMJI ,amesema uchaguzi wa mwaka 2025  fomu ya Ubunge wa Jimbo la Ilala atamlipia Mbunge  wake Mussa Zungu ,katika kinyanganyiro cha uchaguzi mkuu .

Diwani Saady Kimji ,alisema hayo Kata ya Ilala wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi ambapo mgeni rasmi Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ilala Said Sidde  .

"Chama chetu cha Mapinduzi CCM mwaka huu 2025 kinajiandaa na uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani ambapo mimi Diwani wa Ilala Saady Khimji  nitamlipia Mbunge  wangu Mhe Mussa Zungu fomu ya Ubunge mwaka huu, ili agombee ubunge kwa mara nyingine kwa sababu Ilala inamuhitaji kutokana na kazi kubwa ya kimaendeleo aliyoifanya "alisema Khimji. 

Diwani Kimji, alisema awali alikabidhi shilingi milioni 1000,000/= kwa ajili ya kumchangia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kugombea Urais mwaka huu katika uchaguzi mkuu wa vyama vingi wa Rais wabunge na madiwani. 

Alisema wananchi wote wa Ilala tunampigia kula Rais wetu Dkt.Samia amefanya mambo makubwa katika utekelezaji wa Ilani kwa kushirikiana na Mbunge wetu Musa Zungu hivyo wote tunawalipia fomu katika kinyanganyiro hicho.

Alisema kauli mbiu Ilala kumrudisha Dkt Samia kura za ndio alitumia fursa hiyo kumpongeza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde ambapo wajumbe wote wa Wilaya hiyo kura za ndio walimpigia Dkt.Samia kwenye mkutano mkuu wa CCM Taifa uliofanyika Dodoma hivi karibuni. 



Hakuna maoni