Zinazobamba

NAIBU WAZIRI NYONGO ATETA NA AZAKI,FCS YAFUNGUKA

Na Mussa Augustine.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mh.Stanslaus Haroon Nyongo (Mb,)ameziomba Asasi za Kiraia (AZAKI) kufanya majadiliano ya pamoja badala ya kujikita kwenye ukosoaji, ili kujenga uelewa wa pamoja utakaofanikisha upatikanaji wa Dira ya Taifa ya 2050 inayotokana na maoni ya Wananchi pamoja na wadau mbalimbali kama ilivyo dhamira ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Ametoa rai hiyo leo Januari 10,2025  Jijini Dar es salaam, wakati  akifungua mkutano wa Asasi za Kiraia (AZAKI)nchini Tanzania,zilipokutana kufanya  mapitio ya Rasimu ya kwanza ya dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050.

Naibu Waziri Nyongo amesema kwamba wakati akiwa Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma za maendeleo ya Jamii alikutana mara kwa mara na Asasi hizo za kiraia.

"Usipoelewa dhamira yao ya kukumbusha baadhi ya mambo, huenda ukafikiri kuwa wanaikosoa serikali kila wakati jambo ambalo sio la kweli,wanafanya hivyo kwa ajili ya kujenga uwelewa mpana kuhusu masuala mbalimbali wanayojadili" amesema

Nakuongeza kuwa ,sisi kama Serikali tumejiandaa  vya kutosha kusikiliza kila maoni ya Wadau na Wananchi,jambo hilo ni muhimu zaidi ili kuhakikisha kuwa Dira 2050 inakuwa halisi na inayotokana na maoni ya wananchi. "Kwa upande wake Mkurugenzi wa Foundation For Civil Society (FCS) Justice Rutenge amehimiza umuhimu wa  Kukuza uchumi na kuwa na uchumi shindani kuelekea miaka 25 ijayo ili kutoa hakikisho la Nchi kuwa na ustawi Jumuishi na ulio endelevu kwa vizazi na vizazi.

Pia Bw.Rutenge ameishukuru Serikali kuwajumuisha kwenye uandishi wa Dira ya Taifa ya  2050, akihimiza umuhimu wa ushindani kwa ngazi ya ndani ya nchi.

 "Tukianzia na Ngazi ya Mikoa kama ilivyo nchini Kenya ambapo Kaunti mbalimbali zimekuwa zikishindana kwa vigezo vya kutengeneza ajira mpya na ujumuishwaji wa makundi ya pembeni katika ustawi na ukuzaji wa uchumi,hivyo tufanye ushindani kama huu kuanzia ngazi za Mikoa katika nchi yetu ya Tanzania" amesema Rutenge

Hata hivyo Mkuu wa   programu za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, (UNA-TANZANIA) Bw. Lucas Kifyasi,amesema utekelezaji wa dira hiyo utaifanya miaka 25 ijayo wakati ambapo dunia itakuwa imeelekeza nguvu zake kwenye mapinduzi ya viwanda na hivyo suala la elimu litakuwa muhimu zaidi katika kuhakikisha kuwa teknolojia inakuwa thabiti na inayorithishwa kwa vizazi na vizazi.



Hakuna maoni