Zinazobamba

TAMASHA LA KUWAKUMBUKA WASANII WALIOTANGULIA MBELE ZA HAKI LITAKUA ENDELEVU: UWOYA


Na Mussa Augustine 

Muigizaji wa Bongo Movie Irene Uwoya amesema Tamasha la Kuwakumbuka Wasanii Waliotangulia Mbele za Haki linatakiwa kua endelevu ili kuweza Kuwapa heshima Wasanii hao.

Ametoa Matamshi hayo leo Septemba 7,2024 wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika Viwanja wa Leaders Club Jijini Dar es salaam wakati wa Tamasha la Kuwakumbuka Wasanii waliotangulia mbele za haki.

"Tumelifanya kisanaa hivyo tamasha hili naamini litakua endelevu,litatoa heshima kwa Wasanii waliofanya kazi kubwa ya sanaa",amesema Uwoya

Tamasha hilo la aina yake limefanyika nakuhudhuriwa na Wasanii mbalimbali pamoja na wageni waarikwa.




Hakuna maoni