MONALISA AIOMBA SERIKALI KUWEKA MAKUMBUSHO YA KAZI ZA WASANII
Na Mussa Augustine
Serikali imeombwa kuweka utamaduni wa kuweka makumbusho ya kazi za wasanii nchini ili kutoa fursa kwa watu mbalimbali wakiwemo watalii kwenda kuzitazama.
Monalisa ambaye anafanya vizuri katika tasnia ya uigizaji, ametanabaisha kuwa Serikali ikiwekeza zaidi katika makumbusho ya kazi za filamu itafanya kusukuma maendeleo ya tasnia hiyo ambayo imetoa ajira Kwa vijana wengi nchini.
" Ni muhimu kwa Serikali kuangalia kutengeneza nyumba ya makumbusho au maktaba ya kazi za wasanii wa filamu na wanamichezo ili kutoa fursa kwa wananchiI na watalii kutembelea na kuona kazi, zilizofanywa," amesema
Pia amesema licha ya kuwepo Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar es Salaam bado inahitajika kuwepo kwa uwekezaji wa kina ili kupata kuwakumbuka na kuwapa hadhi wasanii waliongulia mbele ya haki, hayo ameyabainisha Leo jijini Dar es Salaam katika Dua ya kuwakumbuka wasanii waliotangulia mbele ya haki.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni